Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa, Akiwa
kwenye viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam, Tayari kwa kuanza
kutembelea mabanda yaliyoko kwenye maonesho ya 43 ya biashara(sabasaba), Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Bwana Edwin Rutegaruka
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent Bashungwa
akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Kuhusu
Maonesho ya 43 ya Biashara (sabasaba) ambayo yalianza Juni 28, 2019 na
yatazinduliwa Rasmi Hapo Kesho na Makamu wa Rais wa Tanzania, Suluhu
Hassan, huku kauli mbiu ikiwa ni “ Usindikaji wa mazoa ya kilimo kwa
maendeleo endelevu ya Viwanda”. 
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa akiwa
katika banda la kampuni ya kutengeneza Majani ya Chai (Chai Bora)
alipokua akitembelea mabanda yaliyoko kwenye maonesho ya 43 ya
biashara(sabasaba), wa pili Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Bwana Edwin Rutegaruka.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa,
akipokea Maelezo kutoka kwa mjasiriamali wa asali ya asili katika
maonesho ya 43 ya biashara(sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya
sabasaba Jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Innocent Bashungwa,
akisikiliza maelezo kutoka kwa Maneja Msaidizi, Idara ya Uhusiano na
Itifaki kutoka Benki Kuu ya Tanzania, Vicky Msina, kuhusu historia ya
Sarafu ya Tanzania, mara baada ya kutembelea katika Banda hilo, kwenye
maonesho ya 43 ya biashara(sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya
sabasaba Jijini Dar es Salaam, Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Bwana Edwin Rutegaruka. 

Elizabeth Daudi kutoka Dodoma Akionesha vitu vya asili katika
kabila la Wagogo katika Maenesho ya 43 ya Biashara (sabasaba) ambayo
yalianza Juni 28, 2019 na yatazinduliwa Rasmi Hapo Kesho na Makamu wa
Rais wa Tanzania, Suluhu Hassan, huku kauli mbiu yake ikiwa “ Usindikaji
wa Mazoa ya Kilimo kwa Maendeleo Endelevu ya Viwanda”. 

Afisa Habari kutoka kituo cha Uwekezaji, Latifa Kigoda, akielezea
huduma ambazo Taasisi hiyo inazitoa kwa wawekezaji katika Maonesho ya 43 ya Biashara (sabasaba) ambayo yalianza Juni 28, 2019 na yatazinduliwa
Rasmi Hapo Kesho na Makamu wa Rais wa Tanzania, Suluhu Hassan, huku
kauli mbiu yake ikiwa “ Usindikaji wa Mazoa ya Kilimo kwa Maendeleo
Endelevu ya Viwanda”. 
Moja ya Bidhaa kutoka katika kampuni ya kuunganisha Matrecta ya
URSUS kama linavyonekana kwenye picha katika maenesho ya 43 ya
Biashara (sabasaba) ambayo yalianza Juni 28, 2019 na yatazinduliwa
Rasmi Hapo Kesho na Makamu wa Rais wa Tanzania, Suluhu Hassan, huku
kauli mbiu yake ikiwa “ Usindikaji wa Mazoa ya Kilimo kwa Maendeleo
Endelevu ya Viwanda”.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...