Moureen Rogath, Buhigwe. 

Mfumo wa utoaji taarifa katika shule za msingi(Shool Information System), umesaidia kupunguza utoro wa wanafunzi katika shule ya msingi Biharu wilayani hapa mkoani Kigoma.

Akizungumza mwalimu mkuu wa shule hiyo Medani Yohana alisema walipokea Kishwambi(Tablet) kutoka Mpango wa Kuinua Elimu ya Msingi(Equip), kwaajili ya kuendeleza mfumo wa takwimu katika shule mbalimbali.

Alisema mfumo huo umewarahisishia kukusanya taarifa za wanafunzi kwa kuongezeka kwa mahudhurio kutoka asilimia 70 kabla na baada kufikia asilimia 95 ya wanafunzi hali iliyopelekea kupunguza utoro katika shule hiyo.

“Baada ya kupata Kishwambi katika shule yetu tuliwapa elimu waalimu jinsi ya kutumia na kupeleka taarifa Wizarani kwa wakati ukitofautisha na awali ambapo tulikuwa tukitumia madaftari kuhifadhia taarifa hali iliyosababisha kutokufika kwa wakati,”alisema Yohana.

Mwalimu wa shule hiyo Andrea Charukula alisema kifaa hicho kimerahisisha ukusanyaji wa taarifa na kwamba serikali iweze kusambaza vifaa hivyo kwa shule zote nchini kwani itasaidia kupunguza changamoto wanazokutana nazo.

Naye mzazi mwenye mtoto katika shule hiyo Alphonce Kamlenga, alisema walipata muamko wa kuwasimamia watoto wao kufika shule bila kukosa na kupunguza utoro kwa baadhi ya awaalimu.

Equip wametoa vishkwambi (Tablet), 20 kwa waratibu elimu kata na 88 kwa waalimu wakuu wa shule za msingi wilayani Buhigwe lengo likiwa ni kuendeleza mfumo wa takwimu katika shule hizo.
Waalimu wa shule hiyo wakiwa na mwalimu mkuu wakiangalia kishwambi (Tablet)waliyopewa katika kuendeleza mfumo wa takwimu katika shule yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...