Na Maureen Rogath, Michuzi TV, Kigoma
Wanafunzi wa shule ya msingi ya Muyegera iliyopo wilayani hapa mkoani Kigoma wanakabiliwa na changamoto ya upungufu wa matundu ya choo, hali inayosababisha kukithiri kwa utoro shuleni hapo.
Hayo yamebainishwa na mwalimu mkuu wa shule hiyo Bw. Issaya Ntahonkiliye wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa miradi iliyotekelezwa na Mpango wa Kuinua Elimu ya Msingi(Equip). Alisema hali hiyo ya kukosekana kwa choo imesababisha wanafunzi kuumwa homa za matumbo na kushindwa kufika shule.
Alisema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 927 ambapo wanatumia matundu ya choo 10, ambapo wanafunzi wavulana wapo 495 wanatumia matundu ya choo chenye matundu matano huku wanafunzi wasichana 452 nao wakitumia idadi hio hio ya matundu ya choo.
“Kwa wastani wanafunzi wetu wanahitaji jumla ya matundu ya choo 25 kwani vilivyopo haviwezi kutosheleza wanafunzi wote. Na wanafunzi wamekuwa wakiomba ruhusa mara kwa mara kutokana na kuumwa matumbo hali inayosababisha ongezeko la utoro,”alisema Ntahonkiliye.
Makamu mkuu msaidizi wa shule hiyo Amani Emanuel, alisema mbali na kuwa na tatizo la matundu ya choo pia wanakabiliwa na upungufu wa madawati ambapo kwa sasa shule nzima ina jumla ya madawati 256 huku dawati moja likikaliwa na wanafunzi wanne hadi watano na wengine wakikaa chini.
“Tumefikia hatua ya wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili tumewawekea utaratibu wa kuingia mchana kwani wakija wote kwa wakati mmoja madarasa hayatatosha kutokana na kukosekana kwa madawati na yanahitajika zaidi ya madawati 300 ambapo kila mwanafunzi ataweza kukaa kwenye dawati,”alisema Emanuel.
Mratibu elimu kata Yared Yowas, alisema Kutoakana na changamoto zinazoikabili shule hiyo walibuni mradi wa mashine ya kusaga na kukoboa pamoja na kuandaa shamba la miti kwa fedha walizopata kutoka kutoka Mpango wa Equip.
Alisema walipata kiasi cha Sh1.5 Milioni kutokana na andiko la mradi wa kuomba fedha ambapo waliweza kununua mashine hiyo na kwamba fedha itakayopatikana iweze kutatua changamoto za shule hiyo.
Alisema walipokea fedha kiasi cha Sh.550,000 kwa ajili ya shuguli za kuingizia kipato shule, ambazo waliweza kuandaa shamba la miti 6,000 kwa sh 350,000 ambapo miti hiyo ikikaribia kuvunwa wataweza kupata kiasi cha zaidi ya Sh.15 milioni.
Mradi wa mashine ya kusaga na kukoboa uliobuniwa na waalimu na wazazi kwaajili ya shule ya msingi Muyegere iliyopo wilayani Buhigwe kwa lengo la kujipatia kipato na kujiendesha yenyewe na kutatuta changamoto zinazowakabili
Mradi wa shamba la miti uliobuniwa na waalimu na wazazi kwaajili ya shule ya msingi Muyegere iliyopo wilayani Buhigwe kwa lengo la kujipatia kipato na kujiendesha yenyewe na kutatuta changamoto zinazowakabili




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...