NA MWAMVUA MWINYI,MAFIA
KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa ,Mzee Mkongea Ali amesita kufungua na kuweka jiwe la msingi miradi mitatu wilayani Mafia ,mkoani Pwani na kutoa wiki mbili kwa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kuchunguza miradi hiyo ,thamani yake halisi na matumizi kisha apelekewe taarifa .
Miradi hiyo ni pamoja na hospital ya wilaya ambayo ilitolewa kiasi cha sh.mil 403.600 .
Mradi mwingine ni ujenzi wa barabara ya KN52 Kilimahewa yenye thamani ya mil.22.336 ambayo kalavati na barabara haina ubora pamoja na uendelevu wa mradi wa maji huko Bweni ambako kero za wananchi hazijafanyiwa kazi kipindi kirefu .
Akielezea juu ya hali hiyo iliyojitokeza ,Mkongea alisema endapo kutabainika kuna ubabaishaji juu ya miradi hiyo basi hatua za kisheria zitachukuliwa.
"Tunapitia miradi hii,tunakagua sio tuu kupitia ila ni kujiridhisha ,hivyo basi TAKUKURU na mkuu wa wilaya fuatilieni suala hili kwa kina ,ili kama kutabainika hakuna ubadhilifu mkuu wa wilaya ataifungua miradi hiyo hapo baadae"alifafanua Mkongea.
Nae mkuu wa wilaya ya Mafia ,Shaibu Nnduma alipokea maelekezo na maagizo waliyopatiwa .Alisema ,jumla ya miradi nane yenye thamani zaidi ya bilioni sita imepitiwa na mwenge wa Uhuru lakini miradi mitatu ndio imewaletea mushkeri.
Mwenge huo baada ya kumaliza mbio zake wilayani Mafia Julai 27 ,umekabidhiwa wilayani Kisarawe na kupokelewa na mkuu wa wilaya hiyo, Jokate Mwegelo Julai 28 na kukimbizwa umbali wa km153.1 .
Akielezea kuhusu miradi iliyopitiwa na mwenge wa Uhuru ,Jokate alieleza miradi mitatu imewekwa jiwe la msingi,minne imekaguliwa na miwili imezinduliwa huku ikiwa imegharimu kiasi cha sh. bilioni 11.97 .#
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...