Na Zainab Nyamka, Michuzi tv
YANGA Tawi la nguvu ya Buku lenye makazi yake Mwananyamala leo wamekabidhi rasmi wodi ya wanaume no. 5 baada ya kuifanyia ukarabati wa ndani na nje ya wodi kwa takribani wiki moja sasa.
Ukarabati huo umefanyika ikiwa ni kuelekea kilele cha siku ya Wananchi inatarajiwa kuadhimishwa na Klabu ya Yanga Jumapili ya Agosti 4,2019.
Akizungumza na Wanahabari mara baada ya makabidhiano Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Mussa Wambura aliwapongeza Wanayanga tawi la Nguvu ya Buku kwa fikra za msaada walioufikiria na fundisho tosha kwa wengine.
Alisema Wambura, msaada wa kitendo mlichokifanya kitabaki kuwa Historia kwa Hospitali ya Mwanabyamala na kuwaomba jamii ziige kutoa misaada ya namna hii inayomgusa kila binadamu kwani Hospitali ni yetu sote tusiiachie Serikali tu, jukumu hili ni la kila mmoja.Leo mmefanya Tawi la Nguvu ya Buku tunaomba wajitokeze na wengine.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Sindano Mwananyamala ambako Tawi hilo linapatikana aliwapongeza sana Tawi la Nguvu ya Buku kwa kitendo cha Kijamii walichokifanya na hakika yeye kama mshabiki wa upande wa pili wamejifunza kitu ambacho kinastahili kuigwa na Mwananchi yeyote anayejitambua.
Aidha, Mwenyekiti wa Nguvu ya Buku, Ally Kuacha aliwapongeza wanachama wake kwa kujitoa mpaka kukamilisha mchakato mzima waliokuwa wamekusudia kuelekea kilele cha siku ya Wananchi na kuwaomba waendelee na mshikamano huohuo siku zote.
Mwisho Katibu wa Tawi la Yanga la Nguvu ya Buku, Juma Lyagala alisema ukarabati huo wa Wodi ya Wanaume umegharimu Shilingi 1,830,000/= ambao ni kupaka rangi ndani na nje, kupaka rangi bati pamoja na kubadilisha nyavu za mbu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...