Na Leandra Gabriel, Michuzi Tv
WIZARA ya Elimu kupitia naibu waziri wa wizara hiyo William Ole Nasha wametoa pongezi kwa mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi (VETA) kwa jitihada wanazoonesha katika kuwainua vijana kwa kuwapa fursa za kujiajiri wenyewe kupitia ubunifu mbalimbali.

Akizungumza Leo katika viwanja vya maonesho ya sabasaba jijini Dar es Salaam mara baada ya kutembelea banda la VETA waziri Ole Nasha amesema kuwa matunda ya mamlaka hiyo ya elimu yanaonekana dhahiri kabisa na Kila mwaka VETA inapiga hatua mbele zaidi katika kuzalisha ajira nyingi kwa vijana.

Amesema kuwa vijana watumie fursa zinazotolewa na mamlaka hiyo kwa kupata ujuzi utakao wawezesha kujiajiri wenyewe kupitia fani za ufundi, upishi, kilimo na ufugaji zinazotolewa na mamlaka hiyo na sio kutegemea kuajiriwa pekee.

Aidha amewapongeza VETA kwa kushinda tuzo mbili katika maonesho hayo ya kibiashara ikiwemo tuzo ya taasisi bora ya elimu katika masuala ya ubunifu na kuwashauri  kuwa ubunifu unaooneshwa na vijana hao usiishie katika maonesho pekee bali wawasaidie kupitia bunifu zao.

Vilevile ameelekeza taasisi zote zinazotoa elimu ya ufundi kubadilisha mitaala ya elimu huku akitolea mfano mabadiliko ya nyaya za umeme ambapo hadi sasa wanafundishwa kupitia mtaala wa zamani licha ya mabadikiko hayo.

Ole Nasha amewaelekeza time ya sayansi na teknolojia nchini (COSTECH) kuwa karibu na wabunifu hao ili waweze kufika mbali zaidi na kueneza na kutumia maarifa yao.
 Gema Ngoo mkufunzi wa masuala ya kilimo akizungumza na Michuzi Tv na kueleza kuwa vijana wasitegee zaidi katika kujiajiri kwani mafunzo yanayotolewa na VETA ni mtaji tosha wa kuweza kujiajiri, leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa elimu William Ole Nasha (kulia) akisikiliza maelekezo kutoka kwa afisa uhusiano wa VETA Sitta Peter (kushoto)  mara baada ya  kutembelea banda hilo katika  viwanja vya mwalimu Nyerere, Leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...