Na Jusline Marco-Arusha
Wanachama wa chama cha wafanyakazi wanahabari Mkoani Arusha wametakiwa kuungana kwa pamoja katika kupigania na kutetea maslahi yao kupitia chama hicho.
Akifunga mafunzo kwa wanahabari wanawake yaliyofanyika Mkoani Arusha Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Arusha Claud Gwandu amewataka wanahabari hao kuwa na ushirikiano katika kutetea maslahi yao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa muda wa Chama cha wafanyakazi kwenye vyombo vya habari Saidi Mmanga amesema kuwa waandishi wengi wa habari wanawake wanakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia,unyanyasaji wa kingono pamoja na mazingira yasiyoridhisha ya kazi hivyo mafunzo hayo yamelenga kuwapa uelewa waandishi hao nakuwakumbusha mikataba mbalimbali ya kimataifa ya masuala ya usawa wa kijinsia kwa wanawake.
Naye mmoja wa waandishi wa habari waliopatiwa mafunzo hayo,Veronica Ignatius akizungumza kwa niaba yao amewataka waandishi wa habari wanawake kufanya kazi kwa malengo na kupiga Vita rushwa ya ngono ili kuweza kuleta mageuzi kwa wengine na kuwa mfano hai kwao.
Hata hivyo mafunzo hayo yameandaliwa na chama cha wafanyakazi wanahabari Tanzania kwa ufadhili wa chama cha wafanyakazi wanahabari kutoka Norway kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya wanahabari (IFS).
Hata hivyo takwimu zinaonyesha kuwa asilimia kubwa ya wanahabari wanawake hawapo katika mazingira bora ya kazi huku maslahi yao ikiwa duni hivyo kupitia mafunzo ya jinsia na usalama kwa wanahabari wanawake mahali pa kazi,wanahabari hao wametakiwa kuungana kwa pamoja ili kuweza kupaza sauti zao.
Waandishi wa habari wanawake Mkoani Arusha wapatiwa mafunzo ya jinsia na usalama mahali pa kazi na Chama cha wafanyakazi wanahabari Tanzania (JOWUTA)



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...