Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa akipata maelezo juu ya gari lililofungwa mfumo wa kutumia gesi asilia wakati alipotembelea banda la Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) lililopo katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Wananchi waliotembelea banda la Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) wakiangalia gari lililofungwa mfumo wa kutumia gesi asilia.
Wafanyakazi wa TPDC wakiwa katika picha ya pamoja Kaimu Mkurugenzi Mhandisi Msomba.
Na Zainab Nyamka, Michuzi TV.
SHIRIKA la maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) wamesema mpaka kufikia mwezi Septemba mwaka huu watakuwa wameshafungua vituo vingi vya huduma ya gesi kwa magari. Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) Mhandisi Kapulya Musomba wakati wa maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
Musomba amesema, mpaka sasa kuna kituo kimoja cha kuuzia gesi ambacho kipo Ubungo ila mkakati wao ni kuwa na vituo vingi sana vitakavyotoa huduma kwa wananchi. "Kuna kituo kimoja cha gesi ambacho kipo Ubungo ila mikakati tuliyokuwa nayo kufikia Septemba mwaka huu tutakuwa na vituo vingi vya kuuzia gesi, " amesema Musomba.
Ameeleza kuwa, TPDC wapo kwenye mkakati wa kuongea na wamiliki wa Mwendokasi na kuwashauri kuleta magari yatakayokuwa yanatumia gesi ili kupunguza gharama za uendeshaji ikiwemo na kushusha bei kwa abiria. Akielezea faida za Gesi, Masumbo amesema mpaka sasa uzalishaji wa umeme unategemea asilimia 50 ya gesi na kupelekea kupungua kwa changamoto ya kukatika kwa umeme.
Musumbo amesema, wameshaanza kusambaza gesi katika maeneo ga Mlalakuma, Mikocheni, Mbezi, Mwenge na wapo kwenye njiani kusambaza Mkoa wa Mtwara na Lindi na hiyo ni kwa matumizi ya kawaida majumbani. Ameshauri, watu kuagiza magari yanayotumia gesi, au yanayotumia vyote ili kupunguza gharama za uendeshaji.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...