Na Woinde shizza Michuzi Tv
Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Themi ,jijini hapa kimewawezesha Kofia Ngumu Madereva pikipiki ( bodaboda) wapatao 100 kwa lengo la kuwanusuru na ajali zisizozalazima ambazo zimekuwa zikisababisha vifo na kupunguza nguvukazi ya taifa.
Akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara wa chama hicho,Mwenyekiti wa CCM kata ta Themi,Thomas Munisi amesema mpango huo umelenga kuondoa changamoto ya kutokuwa na kofia ngumu na kusababisha baadhi ya waendesha pikipiki kukamatwa na askari wa usalama barabarani.
Hatua hiyo iliibuka katika zoezi la kufungua mashina katika kata hiyo, ambapo baadhi ya vijana walionyesha kuwa na changamoto ya ukosefu wa kofia ngumu jambo ambalo chama hicho kililazimika kuwafadhili kupitia mpango wake wa kuwezesha vijana na kuwapatia kofia hizo.
Baadhi ya waendesha pikipiki, Elisha Mbise na simon Swai wamekishukuru chama cha mapinduzi kata ya Themi kwa kuwawezesha kupata kofia ngumu wakidai kwamba zitawasaidia sana katika kujikinga na ajali wakati wakitekeleza mahukumu yao.Katika hatua nyingine Munisi amewaonya wanachama wa chama hicho kuacha kuwabeba baadhi ya wagombea wa CCM kwa maslahi yao kwa kuwa chama hicho kinamfumo mpya wa kupata viongozi wake.
Aidha aliwataka wanachama kuacha tabia ya kutembea na majina ya wagombea mfukoni kwa kuwa kila mwanachama anayetaka kugombea anapaswa kuja ofisini kuchukua fomu.
" ule uongozi wa zamani wa kila mwanachama kuwa na viongozi wake mfukoni kwa sasa hilo halipo na tukigundua kuna mgombea yoyote anatumua wanachama wetu kutaka uongozi tutamfyekelea mbali"Amesema Munisi.
Wakati huo huo Munisi alisema CCM imefanikiwa kuwanyakua baadhi ya wafuasi wa chadema wanaokihama chama hicho akiwemo aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema katika kata hiyo,Elias baada ya kuridhishwa na utendaji Kazi wa CCM chini ya mwenyekiti wake Taifa,Dkt John Magufuli.
Mwenyekiti wa CCM kata ta Themi,Thomas Munisi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...