Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
MADEREVA watakaobeba viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Umoja wa nchi zilizo Kusini Mwa Afrika (SADC) wameaswa kuwa na weledi wakati kuwaendesha viongozi hao.
Hayo ameyasema Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Amani wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ushirikiano wa Kimataifa na Kikanda Stephen Mbundi wakati akifunga mafunzo kwa madereva watakaosafirisha viongozi wa SADC yaliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) jijini Dar es Salaam.
Mbundi amesema mkutano huo ni wa kimataifa Dunia nzima inaangalia hivyo kama nchi haitaki aibu yeyote katika ujio wa viongozi hao ikiwa ni pamoja na kuwa na lugha nzuri katika mawasiliano.
Amesema nchi imewapa heshima madereva katika mkutano huo na kuandika historia kwa nchi katika utoaji wa huduma ya kuwasafirisha na kuongeza kuwa masilahi yao yatalindwa.
Mratibu wa Mafunzo hayo ni Mkaguzi Msaidizi Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Ibrahim Samwix .
Nae Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)Profesa Zakaria Mganilwa amesema kuwa mafunzo hayo ni faida kwa madereva katika mkutano wa SADC.
Amesema kuwa madereva waliopata mafunzo wa uzoefu kilichofanyika ni kuwaongezea maarifa namna kuwa na weledi katika kuwaendesha viongozi wa SADC.
Sehemu ya Madereva waliopata mafunzo kwa ajili kuwabeba viongozi wa SADC.
Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Amani wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ushirikiano wa Kimataifa na Kikanda Stephen Mbundi akimkabdhi cheti mafunzo mmoja wa Madereva watakaobeba viongozi wa Mkutano wa SADC George Mkwakwa yaliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Profesa Zakaria Mganilwa akitoa maelezo wakati wa kufunga mafunzo ya Madereva watakaobeba viongozi wa Mkutano wa SADC yaliyoendeshwa katika Chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani Deus Sokoni akitoa maelezo kuhusiana na usalama wakati kuendesha viongozi wa Mkutano wa SADC wakati wa mafunzo ya madereva yaliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)jijini Dar es Salaam.
.Mratibu wa Mafunzo hayo ni Mkaguzi Msaidizi Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Ibrahim Samwix akiwasikiliza maelezo ya viongozi katika kamati ya usafiri kw viongozi wa SADC.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na madereva na baadhi ya watendaji mara baada ya kufunga mafunzo kwa madereva.
Picha ya pamoja ya Mgeni rasmi na watendaji.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...