ALIYEKUWA Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi pichani, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa mwaka 2014 aliikopesha TFF  USD 258,000 na Sh. Milioni 252 na mwaka 2016 aliikopesha TFF USD 50,000 na Sh. Milioni 74 ambapo jumla zilizopo kwenye rekodi ya mahakama ni USD 298,000 na sh.milioni 320.

Aidha Malinzi amedai kuwa, utaratibu wa watu kuikopesha TFF ulikuwepo tokea miaka ya nyuma na kwamba katika kipindi chake walikuwepo  watu mbalimbali ambao walikuwa wakiikopesha TFF, lakini  yeye ndiye Rais wa kwanza kushtakiwa na kufikishwa mahakamani. 

Malinzi amedai hayo leo Agosti 27,2019  mahakamani hapo  wakati akiendelea kutoa utetezi wake dhidi ya kesi inayomkabili ya matumizi mabaya ya madaraka, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji fedha,

Akiongozwa na wakili wake Richard Rweyongeza mbele ya Hakimu Mkazi Maira Kasonde , Malinzi amedai,  fedha hizo alikuwa akiikopesha TFF bila masharti yoyote wala kudai riba na kuongeza kuwa alikuwa akilipwa kadri ambavyo hali ya kifedha ilivyokuwa inaruhusu katika shirikisho hilo ambapo alikuwa analipwa fedha hizi kadiri hali ya kifedha ilivyokuwa inaruhusu pale TFF,  pia nilikuwa nalipwa kwa mafungu yaani kidogo kidogo. 

Amedai Ahamed Mgoyi ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya TFF ni miongoni mwa watu ambao walikuwa wakilikopesha shirikisho hilo kwa muda mrefu na hilo limethibitishwa mahakamani hapo na Shahidi wa sita Daniel Msangi iliyethibitisha na kutambua malipo ya Sh. Milioni 55 ambayo aliikopesha TFF na kulipwa. 

"Na katika maombi ya hati ya risiti tuliomba maelezo ya Mgoyi ili kuona anamdai nani mpaka sasa,  hadi upande wa mashtaka unafunga ushahidi wake,  mimi sikupatiwa hiyo nyaraka kuangalia, " alidai Malinzi. 

Alidai Mgoyi alikuwa akiikopesha TFF kwa kutumia utaratibu aliyokuwa akiufanya yeye wa bila kuweka masharti yoyote. 

Aidha Malinzi alidai kuwa yeye na wenzake walikamatwa Juni 27, 2017 na kulazwa mahabusu ya Polisi siku mbili lakini Juni 29 mwaka huo walipelekwa mahakamani na kunyimwa dhamana. 

"Wakati nakamatwa nilikuwa najiandaa kufanyiwa usahili mimi na wagombea wenzangu tuliokuwa tukigombea nafasi za uongozi TFF ikiwemo urais, " alidai Malinzi. 

Alidai baada ya kunyimwa dhamana,  Julai Mosi, 2017 kikao cha dharura cha kamati ya utendaji ya TFF kiliitishwa na kumkaimisha urais wa TFF Wallace Karia kisha kuvunja kamati ya uchaguzi iliyokuwepo hapo awali na kuundwa nyingine mpya ambayo iliondoa jina lake miongoni mwa wagombea urais. 

"Kwa hiyo Wallace Karia na wagombea wengine walipitishwa kugombea bila jina langu kuwepo,  hata hivyo kwa mujibu wa katiba ya TFF mwenye mamlaka ya kuitisha kikao cha dharura cha kamati ya utendaji wa TFF ni rais hivyo kukaa kwangu mahabusu hakukuniondolea sifa ya kuwa mjumbe wa kikao hicho, kwahiyo kanuni zilivunjwa pamoja na katiba pia ilivunjwa, " alidai Malinzi. 

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mhasibu wa TFF Nsiande Mwanga, Karani Flora Rauya na Selestine Mwesigwa.

Malinzi, Mwesigwa na Nsiande wapo rumande kwa kukabiliwa na mashtaka ya utakatishaji wa fedha kuwa miongoni mwa mashtaka  ambayo kwa mujibu wa sheria hayana dhamana huku Frola akiwa  nje kwa dhamana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...