Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), yashiriki maonesho ya 27 ya
wakulima, wavuvi na wafugaji yanayoadhimishwa kitaifa katika viwanja vya
Nyakabindi, wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Maonesho hayo yenye kauli mbiu
‘Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa Ukuaji wa Uchumi wa Nchi’ yamelenga kutoa
fursa kwa taasisi mbalimbali nchini za serikali na binafsi kutoa elimu hasa ya
teknolojia wanazozitumia na namna zinavyoweza kuwasaidia wakulima katika
kurahisisha utekelezaji wa majuku yao ya kila siku ya kilimo, ufugaji na uvuvi.
Meneja Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Bi. Julien Mafuru
ameeleza kuwa NIDA imeshiriki kwenye maonesho ya Nanenane mwaka huu
ili kutoa fursa kwa wakulima, wafugaji na wavuvi Kusajiliwa kwa ambao
hawajawahi Kujitokeza Kusajiliwa popote nchini, waombaji kuangalia taarifa
za maombi ya Usajili yalikofiki kwa waliokamilisha Usajili, Elimu juu ya namna
ya kupata Nakala ya Kitambulisho cha Taifa kupitia tovuti ya NIDA
( www.nida.go.tz ), Matumizi ya Namba ya Utambulisho (NIN) na Kitambulisho
cha Taifa, kukusanya maoni ya wateja kwa lengo la kupata mrejesho juu ya
huduma zetu, kutangaza njia zetu mbalimbali tunazotumia kuwasiliana na
wananchi pamoja na kutangaza ofisi zetu za Usajili zilizopo katika kila wilaya
nchini.
Bi. Mafuru ameeleza kuwa mwitiko wa wananchi ni mkubwa hasa kundi la
watu ambao waliokamilisha Usajili siku za nyuma, wengi wamefika katika
banda la NIDA Na. 7 kwenye viwanja vya Nyakabindi na kupatiwa namba zao
za Utambulisho wa Utaifa (NIN) kwa ambao zimeshatoka. Namba hizo
zimewasaidia kutambulika na kuweza kufika pia katika mabanda ya wadau
wetu walioko katika maonesho haya ili kupata huduma nyingine za kijamii na
kiuchumi kama vile kusajili laini, kukata TIN, kufungua akaunti ya benki,
kupata mkopo kwenye SACCOSS n.k.
Kwa Upande wake Bi Fatuma Odoyo, mwananchi mkazi wa Bariadi
ameishukuru serikali ya awamu ya 5 kupitia NIDA kwa kusogeza huduma
karibu na wananchi kupitia kutoa huduma za Usajili kwenye maonesho ya
Nanenane kwani alikuwa bado hajafika kwenye ofisi za Usajili za NIDA kupata
huduma hiyo.
’Ndani ya maonesho haya niliposikia matangazo kwenye redio
kuwa NIDA wapo nikafika kwenye banda lao na kuanza Kujisajili kwani
nahofia laini yangu ya simu kufungwa muda wa ukomo ukifika wa kutakiwa
kusajili laini ya simu kwa kutumia alama za kibaiolojia ambapo wanatuhitaji
tuwe na namba ya NIDA’ Bi Fatuma amesema.
Mmoja wa wananchi wa Mkoa wa Simiyu aliyejitokeza kujiandikisha ili kupata Kitambulisho cha Taifa akijaza fomu ya usajili.
Bi Careen Kuwite Afisa Msajili Mkoa wa Simiyu ameeleza kuwa wananchi
hususan kundi la wakulima, wavuvi na wafugaji wanapotambuliwa katika
mfumo wa Utambuzi unaosimamiwa na NIDA na kupatiwa Namba ya
Utambulisho, kunawawezesha kupata huduma za kijamii kirahisi kama vile
kupata ruzuku za pembejeo za kilimo, kusajili laini ya simu, kujisajili kwenye
vyama vya ushirika (kwa wakulima, wavuvi na wafugaji), kufungua akauti ya
benki, kupata msaada wa TASAF unaotolewa kwa kaya masikini, hati miliki ya
kiwanja na nyumba, hati ya kusafiria ya kielekroniki, kusajili biashara na
kampuni brela, kukata leseni ya udereva, kukopesheka kirahisi kwenye taasisi
za fedha, kupata mkopo wa elimu ya juu kwa wanafunzi, kuomba ajira,
malipo ya pensheni pamoja na huduma nyingine nyingi.
Baadhi ya Wananchi wa Mkoa wa Simiyu wakiendelea kupatiwa huduma ya kujisajili ili wapate vitambulisho vya taifa, walipotembelea banda ya NIDA katika maonyesho ya Nane Nane yanayoendelea katika uwanja wa Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu leo.
Akihitimisha Bi. Julien amewasihi wakulima, wavuvi, wafugaji na wananchi
wote kiujumla kujitokeza Kusajiliwa kwa wingi ili kupata Namba ya
Kitambulisho cha Taifa kwa wakati.
Aidha ameeleza kuwa wananchi
watakaoshindwa kutumia fursa ya Kusajiliwa kwenye maonesho haya ya 27 ya
Nanenane wafike kupata huduma katika ofisi za Usajili za NIDA zilizoko katika
kila wilaya nchi nzima wakiwa wamekamilisha kujaza fomu za Usajili
zinazopatikana serikali za mitaa, kwenye tovti ya NIDA na kwenye ofisi za
Usajili za NIDA.








Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...