Na Zainab Nyamka, globu ya Jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaondolea mashtaka mawili ya utakatishaji, kati ya kumi yaliyokuwa yakiwakabili aliyekuwa rais wa club ya Simba Evans Aveva na Makamu wake Godfrey Nyange Kaburu baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka hayo dhidi yao.
Hata hivyo, washtakiwa hao pamoja na aliyekua ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Zacharias Hansppope wamekutwa na kesi ya kujibu katika mashtaka saba ambayo ni kughushi, kula njama, matumizi mabaya ya madaraka, kutoa nyaraka za uongo, na kutoa maelezo ya uongo ambayo upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa
Kufuatia kuondolewa kwa shtaka hayo ya utakatishaji washtakiwa wamepatiwa masharti ya dhamana kwa sababu mashitaka ya utakatishaji fedha ambayo yaliwanyima dhamana hayapo
Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.
Akisoma uamuzi huo, hakimu Simba amesema ni jukumu la upande wa mashtaka kuthibitisha mashtaka yote kwa washitakiwa na kila shtaka linatakiwa kuthibitishwa peke take na sio kwa kutegemeana.
"Baada ya kuchambua ushahidi wa mashahidi 10 wa upande wa mashitaka, ukiacha shtaka la tano na sita mahakama imeona kuwa washtakiwa wanakesi ya kujibu katika shtaka la 1,2,3,4,7,8 na 9 isipokuwa katika shitaka la tano na sita na ambayo shtaka la utakatishaji linaondolewa" amesema hakimu Simba.
Kufuatia kuondolewa kwa mashtaka hayo, Wakili wa washtakiwa hao Nehwmia Nkoko aliiomba mahakama kuwapatia wateja wake dhamana kwani mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo yaliyokuwa yanawanyima dhamana washitakiwa hayapo.
Wakili wa Takukuru, Leornad Swai alipoulizwa kama ana pingamizi lolote juu ya dhamana alidai hawana pingamizi ambapo Hakimu Simba aliwapatia masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini 2 watakaosaini bondi ya Sh.Mil 30 kwa kila mmoja pamoja na kuwa na vitambulisho
Kesi hiyo imeahirishwa hadi leo Septemba 20, 2019 kwa ajili ya washitakiwa kuanza kujitetea.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...