Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza Dkt. Phillis Nyimbi
mwishoni mwa wiki alizindua msimu wa kumi wa mbio ndefu za Rock City
Marathon 2019 kwa jiji la Mwanza huku akionyeshwa kuridhishwa na
maandalizi ikiwemo zawadi na ubora wa medali zitakazotolewa kwa washindi
na washiriki wa mbio hizo.
Mbio za Rock City Marathon zinatarajiwa kufanyika Octoba 20, mwaka huu kwenye viunga vya jengo la kibiashara la Rock City Mall lililopo jijini Mwanza ambapo zaidi sh Mil 30 zitatolewa kwa washindi sambamba na fulana pamoja na medali.
Uzinduzi huo ulishirikisha wadau mbalimbali wa mbio hizo, wakiwemo viongozi kutoka Serikalini, Viongozi kutoka Taasisi mbalimbali, Wadhamini wa mbio pamoja na baadhi ya wanariadha kutoka vilabu vya mchezo huo jijini Mwanza.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela, Dkt. Nyimbi mbali na kuwapongeza wadau hao kwa maandalizi mazuri ya mbio hizo pia alithibitisha ushiriki wake pamoja na ushiriki wa Mkuu wa Mkoa huo Bw John Mongella sambamba na viongozi waandamizi wa mkoa huo kwenye mbio hizo zenye umaarufu mkubwa katika ukanda wa Ziwa.
"Kwa kuzingatia ubora wa maandalizi pamoja na uzito wa malengo ya mbio hizi nitamke bayana kuwa Serikali ya Mkoa wa Mwanza tupo tayari kushirikiana na waandaaji wa mbio hizi si tu kwa kushiriki bali pia kuhakikisha kwamba mwaka huu mbio hizi zinafana na zinavutia washiriki wengi zaidi hususani wa kimataifa,'' alisema Dk Nyimbi.
Mbio za Rock City Marathon zilizoanzishwa miaka kumi iliyopita zimezidi kujiongezea umaarufu kila mwaka na tayari zimefanikiwa kuwavutia baadhi ya wadhamini ikiwa ni pamoja na kampuni za TIPER, Pepsi, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA).
Wadhamini wengine ni pamoja na kampuni ya uwakili ya Lis Law Chambers & Consultants, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), CF Hospital, Metro FM, Mwanza Water, Pigeon Hotel, Kampuni ya Usafi ya SDN na Kampuni ya Ulinzi ya Garda World.
Kwa upande wake Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI) Bi Magdalena Laizer mbali na kuwashukuru wadau wa mbio hizo wakiwemo wadhamini alitoa wito kwa washiriki wa ndani hususani wa mikoa ya Kanda ya Ziwa pamoja na wadhamini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mbio hizo ambazo kwa mwaka jana zilifanikiwa kuhusisha washiriki zaidi ya 1200.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Mshauri wa masuala ya Ufundi wa mbio hizo Bw John Bayo alisema maandalizo ya mbio hizo kwasasa yamekamilika kwa asilimia 70 huku akitumia fursa hiyo kutangaza njia zinakazotumika wakati wa mbio hizo zinazohusisha mbio za 42 km, 21 km, 5 km na 2.5 km.
Alisema kwasasa usajili wa mbio hizo unaendelea kupitia vituo mbalimbali katika mikoa ya Mwanza (Rock City Mall, Pasiansi Afro Twist Gym), Dodoma (Shabiby Bus Terminal), Dar es Salaam (Shamo Tower na Imalaseko Super Market), Arusha pamoja na Bagamoyo mkoani Pwani.
“ Pia usajili unaweza kufanyika kwa njia ya mtandao kupitia website yetu ya Rock City Marathon,’’ alitaja.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza Dkt. Phillis Nyimbi (katikati) akionyesha moja ya medali itakayotolewa kwa washindi na washiriki wa mbio za Rock City Marathon 2019 wakati wa hafla fupi ya uzinduzi rasmi msimu wa kumi wa mbio hizo kwa jiji la Mwanza iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini humo. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mshauri wa masuala ya Ufundi wa mbio hizo Bw John Bayo (kulia) na Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI) Bi Magdalena Laizer (kushoto).Mbio hizo zinatarajiwa kufanyika Octoba 20, mwaka huu kwenye viunga vya jengo la kibiashara la Rock City Mall lililopo jijini Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza Dkt. Phillis Nyimbi (alievaa suti nyeusi) akifungua pazia kuashiria uzinduzi rasmi msimu wa kumi wa mbio ndefu za Rock City Marathon 2019 kwa jiji la Mwanza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi huo iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini humo. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI) Bi Magdalena Laizer (wa kwanza kushoto) na wadau mbalimbali wa mchezo huo jijini humo. Mbio hizo zinatarajiwa kufanyika Octoba 20, mwaka huu kwenye viunga vya jengo la kibiashara la Rock City Mall lililopo jijini Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza Dkt. Phillis Nyimbi (alievaa suti nyeusi) akifurahia muonekano wa medali pamoja na ramani ya njia zitakazotumika kwenye mbio za Rock City Marathon 2019 wakati wa hafla fupi ya uzinduzi rasmi msimu wa kumi wa mbio hizo kwa jiji la Mwanza iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini humo. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mshauri wa masuala ya Ufundi wa mbio hizo Bw John Bayo (kushoto kwake) na wadau mbalimbali wa mchezo huo jijini humo. Mbio hizo zinatarajiwa kufanyika Octoba 20, mwaka huu kwenye viunga vya jengo la kibiashara la Rock City Mall lililopo jijini Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza Dkt. Phillis Nyimbi (kulia) akionyesha fomu ya usajili wa mbio za Rock City Marathon 2019 kuthibitisha ushiriki wake kwenye mbio hizo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi rasmi msimu wa kumi wa mbio hizo kwa jiji la Mwanza iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini humo. Kushoto ni Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI) Bi Magdalena Laizer. Mbio hizo zinatarajiwa kufanyika Octoba 20, mwaka huu kwenye viunga vya jengo la kibiashara la Rock City Mall lililopo jijini Mwanza.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza Dkt. Phillis Nyimbi (kulia) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla fupi ya uzinduzi rasmi msimu wa kumi wa mbio za Rock City Marathon kwa jiji la Mwanza iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini humo.
Mshauri wa masuala ya Ufundi wa mbio hizo Bw John Bayo akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla fupi ya uzinduzi rasmi msimu wa kumi wa mbio za Rock City Marathon kwa jiji la Mwanza iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini humo.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza Dkt. Phillis Nyimbi (mwenye suti nyeusi) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa mbio za Rock City Marathon wakiwemo viongozi kutoka Serikalini, wadhamini wa mbio hizo pamoja na wawakilishi wa washiriki wa mbio za watoto (waliovaa nguo nyekundu) wakati wa hafla fupi ya uzinduzi rasmi msimu wa kumi wa mbio za Rock City Marathon kwa jiji la Mwanza iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini humo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...