Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania (IGP) Simon Sirro akizungumza na baadhi ya Askari mkoani Arusha alipowatembelea sambamba na kukabidhi nyumba kwa askari hao.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza na baadhi wa Askari wa Jeshi la Polisi Njiro mkoani hapo kabla ya kukabidhi nyumba kwa askari sita
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro akisisitiza jambo kwa baadhi ya Askari katika mkoa wa Arusha
Mmoja wa kiongozi wa Askari wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha akizungumza jambo kabla ya IGP kukabidhi nyumba kwa baadhi ya askari.
Mmoja wa Askari wa Jeshi la polisi mkoa wa Arusha kati ya sita Arusha akikabidhiwa funguo za nyumba na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,Kushoto kwake ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro,Kulia kwake ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Shanna.
Na Vero Ignatus,Arusha
Mkuu wa Jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka jeshi la polisi nchini kuzingatia nidhamu wawapo kazini sambamba na kutojihusisha na mambo ya kisiasa badala yake wafanye kazi kwa uadilifu sambamba na kusimamia sheria kama kazi kubwa ya jeshi
Amewasisitizia kuiheshimu kazi kujiamini na kusimamia sheria ,amesema askari ayupo upande wa siasa bali kutambua kuwa wajibu mkubwa wa askari ni kusimamia sheria na kuwatumikia watanzania,amesema aslani hapendi kumfukizisha kazi askari ila askari pia asilmazimishe kumfukuza amemtaka kila askari kutimiza wajibu wake.
"Hapa hakuna baba kanituma hiyo biashara haipo mmenipata vizuri!kila mmoja wenu atimize wajibu wake kwa mujibu nwa sheria "alisema Sirro.
Akizungumza na baadhi ya askari Mkoa wa Arusha Sirro amesema hali ya usalama wa nchi ipo vizuri, amesema changamoto waliyonayo kunaosumbua umebakia mdogomdogo,changamoto zilizopo ni dalili za ugaidi na baadhi ya askari kutoa siri za jeshi.
IGP Sirro amesema serikali ametatua changamoto iloyokuwa inawakabili ya sare kwakutoa jumla ya shilingi Bil.10 sambamba na shilingi kwaajili ya bil 3.5 kwaajili ya manunuzi ya hekopta ya jeshi
Amesema hapo miaka ya nyuma walikuwa na tatizo la sare ila kwa sasa wanakwenda vizuri kwani wameshachukua hatua ambapo kila mkoa atanunu vyerehani na kuhakikisha kila mkoa utahakikisha askari wanashonewa na watakuwa na mafundi wao.
Amesema shida kubwa inayolisumbua jeshi la polisi kwa sasa ni baadhi ya askari wachache wanaowauzia askari wenzao sare za jeshi hilo jambo ambalo linapelekea kuleta chuki miongoni mwa askari
“Kama kuna mjinga anataka aende kwa shangazi yake aendelee kuuza uniform,aendelee kununua uniform nimekwenda Zanzibar nimewaambia,na ninavyosema hivi kuna wengine wapo mahabusu kwa sasa unapomuuzia mwenzako uniform unategemea nini unapochukua fedha ya askari mwenzako unamuuzia government stoo maana yake nini’’aliuliza Sirro.
Amesema kuna baadhi ya askari wanatamaa na wanadhani zitawasaidia badala yake zitawapeleka pabaya amesema Jeshi lazima wapendane huku akiwasisitizia kwamba kama wanapendana hawawezi kuuziana sare hizo
Pia amewapongeza kwa nyumba nzuri amesema tayari zilishafanyiwa uzunduzi Geita nyumba 400 na Rais wa Jamuhuri hivyo amewataka askari 6 ambao wamekabidhiwa nyumba hizo maeneo ya njiro wazitunze ili zidumu
Ndiyo maana nikiwaona wenzetu wa bendi wanancheza naona ni kipaji wamepewa na Mungu wewe ukiona siyo kazi shauri lako na Rais Magufuli kule Geita.Kwa upande wake mkuu wa moa wa Arusha Mrisho Gambo amesema Gambo amesema serikali ngazi ya mkoa wameweka mkakati endelevu wa kujenga nyumba moja ya jeshi la polisi itakayokaliwa na familia 6 u wa mkoa Mrisho Gambo amelipongeza jeshi la polisi mkoani Arusha ambapo "Jeshi hilo ndilo limbiliao la wananchiwanyonge,wenye uwezo na wananchi wa makundi yote kayika Taifa la Tanzania"Alisema Gambo
Gambo amesema jeshi la polisi amesema kwa kupitia jeshi hilo mkoa huo umekuwa salama kwani limekuwa likilinda usalama wa raia na mali zao na linahusika na maswala ya mkoa kwa asilimia kubwa,amesema yapo majeshi yanafanya kazi kubwa na mzuri ,ila jeshi linaloonekana mara kwa mara mbele ya raia ni jeshi la polisi.
Aidha amelitaka jeshi hilo kuhakikisha raia wanakuwa salama na mali zao katika maeneo yao kipindi chote cha uchaguzi wa serikali za mtaa ,bila kujali itikadi za vyama vyao, huku wakikumbuka wajibu wa polisi ni kusimamia sheria na hawafungamani na siasa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...