Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv
MWANDISHI wa Habari Erick Kabendera àmeielezea mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa amepata huduma za Kitabibu katika Hospitali ya Amana na katika uchunguzi wa awali uliofanyika madaktari wamebaini kuwa anamatatizo katika pingili za mgongo.

Amedai kuwa jana (Septemba 17,2019) alipelekwa katika Hospitali ya Amana ambapo alifanyiwa vipimo vya X-ray, damu pamoja na vipimo vingine lakini bado anasubiri majibu ili apatiwe màtibabu.

"Mheshimiwa hakimu, nashukuru nimepata huduma ya kitabibu, vipimo vya awali vinaonesha ninatatizo katika pingili za mgongo, lakini bado nina maumivu makali, vipimo zaidi vimefanyika ili kubaini kama ninamatatizo zaidi na majibu yake nitapewa mwishoni mwa wiki hii" amedai mshtakiwa Kabendera.

Mshtakiwa Kabendera ameeleza hayo leo Septemba 18,2019 mbele ya Hakimu Mkazi Agustino Rwezile wakati kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa upelelezi bado haujakamilika

Baada ya kueleza hayo wakili wake Jebra Kambore ameuomba upande wa mashitaka kuharakisha upelelezi wa kesi hiyo. Kesi imeahirishwa hadi Oktoba mosi mwaka huu mshtakiwa amerudishwa rumande.

Katika kesi hiyo,Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashitaka matatu likiwemo la utakatishaji wa zaidi ya sh milioni 173.
Katika shitaka la kwanza ilidaiwa kuwa katika kipindi hicho, Kabendera alijihusisha  na mtandao wa kihalifu kwa kutoa msaada kwa genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.

Shitaka la pili ilidaiwa kuwa katika kipindi hicho,bila ya sababu,alikwepa kodi ya sh. 173,247,047.02 ambayo ilitakiwa ilipwe Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Katika shitaka la tatu, kabendera anadaiwa kutakaisha sh.173,247047.02 huku akijua fedha hizo ni mazalia ya kosa la kujihusisha na genge la uhalifu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...