Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha 

Mahakama ya kimataifa inayoshughulikia masuala yaliyosalia ya mahakama za makosa ya jinai, imeanza kusikiliza shauri la aliyekuwa waziri wa mipango wa nchini Rwanda Augustin Ngirabatware aliyehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa makosa matano likiwepo la kuhusika na mauaji ya Kimbari.

Shauri lililosomwa katika mahakama hiyo iliyopo Arusha , pamoja na mambo mengine linaeleza kuwa watu waliotoa ushahidi dhidi ya Ngirabatware walishawishiwa ili waseme uongo mahakamani.

Mmoja wa mashahidi hao ameiambia mahakama kuwa wakati anatoa ushahidi miaka 10 iliyopita, alikuwa amehukumiwa kifungo cha kunyongwa na hivyo alishawishiwa atoe ushahidi wa uongo mahakamani ili apunguziwe adhabu.

Mwaka 2012, Ngirabatware alihukumiwa kifungo cha miaka 35 Jela na mahakama ya kimataifa ya mauaji ya Kimbari ya nchini Rwanda baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika katika mauji ya kimbari kwa kushirikiana na kundi la mauaji ya halaiki la nchini humo Interahamwe , pamoja na kosa la ubakaji.

Mwaka 2014, Mahakama ya rufaa ya Rwanda ilimpunguzia adhabu ya kifungo kutoka miaka 35 hadi 30 baada ya kuondoa kosa la ubakaji ,kifungo ambacho anakitumikia hadi sasa.Hukumu ya kesi ya Ngirabatware inatarajiwa kutolewa baada ya kukamilika kwa shauri hilo siku ya tarehe 27 ya mwezi huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...