Naibu Waziri wa Kilimo, Husein Bashe amesema moja ya vikwazo vilivyokuwa vinasababisha Sekta ya Kilimo kuendelea ni pamoja na Migogoro na kesi za muda mrefu dhidi ya Makampuni za Kilimo ambapo Serikali imedhamiria kufuta kesi zote ili Kampuni hizo ziweze kununua Mazao
Bashe amesema kampuni zilikuwa zikidaiwa zaidi ya Tsh. Trilioni 10 na serikali hali ambayo ilikuwa inasababisha kushindwa kwenda kutoa huduma kwa wakulima
Aidha, amesema wamekubaliana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwa ndani ya siku 90 Kuanzia leo Septemba 4 suala la madai kwa Kampuni 4 za Kilimo litakuwa limeisha ili kampuni hizo ziendelee kununua mazao kwa wakulima.
Pia, amesema kuna zaidi ya kilo Milioni 12 za Tumbaku zipo mikononi mwa Wakulima na kampuni za kilimo chini ya Bodi ya Tumbaku Tanzania zitakutana na wakulima kununua kilo hizo kuanzia Septemba 12.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...