Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv,

IKIWA ni siku ya tano tangu Rais John Magufuli atoe ruhusa kwa mahabusu wa kesi za uhujumu uchumi kukiri makosa yao na kulipa vigogo Kampuni ya Mawasiliano ya Six Telecoms Limited, akiwemo Wakili maarufu Dk Ringo Tenga, wameandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) yenye maombi mbalimbali kuhusu kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mbali na Tenga, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Hafidhi Shamte au Rashidi Shamte ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni wa hiyo, Mfanyabiashara na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Peter Noni, Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo Noel Chacha na Kampuni ya Six Telecoms.

Mapema, wakili wa Serikali, Jacqueline Nyantori alidai jmbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa shauri hilo leo Septemba 27, limekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba katika ahirisho lililopita, upande wa utetezi uliomba kujadiliana na wateja wao.

Wakili wa Utetezi, Bryson Shayo amedai mahakamani hapo kuwa, wameshauriana na wateja wao na katika mashauriano hayo washitakiwa wameandika barua kwa DPP kuzingatia agizo hilo la Rais John Magufuli la Septemba 22, mwaka huu.

Amedai Septemba 26, mwaka huu washitakiwa hao waliandika barua kwenda kwa DPP yenye maombi mbalimbali kuhusu shauri hilo hivyo, aliomba ahirisho la siku 14 ili barua iweze kujibiwa. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 11 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa wamerudishwa rumande kwa sababu mashitaka yanayowakabili hayana dhamana kisheria.

Septemba 24 mwaka huu upande wa utetezi uliomba mahakama kuitisha shauri hilo leo (jana) kwa sababu ya mazingira ya kesi yenyewe wanaomba wazungumze na wateja wao.Dk Tenga na wenzake wanadai kuwa, kati ya Januari 1, 2014 na Januari 14,2016 Dar es Salaam, walitoza maalipo ya mawasiliano ya simu za kimataifa chini ya kiwango USD 0.25 kwa dakika kwa lengo la kujipatia faida.

Pia katika kipindi hicho, wanadaiwa kuhujumu miundombinu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kutoza gharama chini ya kiwango na kushindwa kulipa USD 3,282,741.12 kwa TCRA, kama malipo ya mapato.

Pia wanadaiwa katika kipindi hicho walishindwa kulipa ada za udhibiti USD 466,010.07 kwa TCRA.

Vile vile ,washitakiwa hao wanadaiwa kuwa waliisababishia TCRA hasara USD 3,748,751.22 sawa na Sh bilioni nane .


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...