Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeelezwa kuwa, maafisa wa Takukuru walimkuta Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Samson Mahimbo (68) akijiandaa kufanya ngono na mwanafunzi wake.

Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Faraja Sambala ameeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi wakati akimsomea mshtakiwa huyo maelezo ya awali ya mshitakiwa.

Akisoma maelezo hayo, Sambala amedai kuwa Mahimbo ni mkazi wa Makongo juu Dar es Salaam na wakati wa tukio alikuwa mwajiriwa wa NIT akifundisha somo la usimamizi wa Barabara na Usafirishaji na kwamba Victoria Faustine alikuwa miongoni mwa wanafunzi wake.

Amedai Januari 11, mshtakiwa Mahimbo alimpigia simu mwanafunzi Huyo akimsisitiza wakutane siku iliyofuata ambapo walikutana baa iitwayo Shani iliyopo maeneo ya Mwenge.

Walipokutana , mshitakiwa alikuwa na mtihani wa marudio ambao Victoria alitakiwa kufanya, karatasi ya majibu na marking scheme ambapo alimsahihishia na kumpa alama 67 na baada ya kumaliza wakuhamia kwenye baa na nyumba ya kulala wageni inayoitwa Camp David , iliyopo Mlalakuwa Mwenge.

Amedai wakiwa pale walikunywa na kulewa kisha wakachukua chumba na kuingia ndani na kwamba mshitakiwa alianza kuvua nguo na kubaki na nguo ya ndani.

"Mshitakiwa alianza kumkumbatia Victoria na kuanza kumvua nguo zake na mara walisikia mlango ukigongwa na Victoria aliufungua na kuingia maofisa wa Takukuru, muhudumu wa baa na mjumbe. Walikuta nguo zipo juu ya meza," alidai.

Mshtakiwa alikamatwa na Januari 12, 2017 alienda kuandika maelezo Takukuru na Agosti 14, mwaka huu aliletwa mahakamani.Mshitakiwa alikana maelezo hayo na kukubali majina yake na mahali anapokaa.

Upande wa mashitaka ulidai kuwa wanamashahidi sita na vielelezo saba ili kuthibitisha mashitaka hayo huku mshitakiwa huyo alidai atakuwa na mashahidi wanne.

Maimu alifikishwa mahakamani hapo akikabiliwa na mashitaka ya kuomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wa chuo hicho.Mhadhiri huyo anadaiwa akiwa mwajiriwa wa NIT alikuwa akifundisha wanafunzi wa muhula wa kwanza wa masomo wa mwaka 2015/16.

Anadaiwa alitenda kosa hilo Januari 12, mwaka 2017 katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Camp David

Ilidaiwa kuwa mshitakiwa huyo akiwa mwajiriwa wa NIT katika kozi ya Usimamizi wa Barabara na Usafirishaji namba LTU 07101 alitumia mamlaka yake alimlazimisha mwanafunzi huyo kutoa rushwa ya ngono.Ilidaiwa kuwa, aliomba rushwa hiyo ili aweze kumfaulisha katika mtihani wake wa marudio katika kozi ya Usimamizi wa Barabara na Usafirishaji uliokuwa unafanyika Januari 5 ,mwaka 2017.

Mshitakiwa yupo nje kwa dhamana na keshi itaanza kusikilizwa Novemba 11, mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...