Mwanamitindo na muziki wa kizazi kipya nchini, Hamisa Mobeto.

Na.Khadija seif, Michuzi TV
STAA wa mitindo pamoja na muziki wa kizazi kipya nchini, Hamisa Mobeto amesema kwa sasa hana muda wa kuongeza mtoto mpaka atakapofunga ndoa.

Mobeto alisema hayo baada ya kuulizwa kama ataongeza mtoto mwingine kwa ajili ya kuongeza familia.

"Kwa sasa sina muda wa kuongeza mtoto zaidi ya kuangalia masuala ya kazi zangu jinsi ya kupata soko ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kupata riziki," alisema Mobeto.

Alisema muda aliokuwa nao kwa sasa ni kuangalia familia yake na kuendesha biashara zake za ushonaji nguo ili aweze kuwavalisha watu maarufu.

"Natamani kuwavalisha watu maarufu ndani na nje ya nchi ili niongeze soko la ubunifu wa nguo na kuunganisha urafiki baina yangu na wateja ambao wanafanya kazi na Mimi," alisema Mobeto.

Staa huyo aliwata mashabiki zake waendelee kumshika mkono kwa kazi anazofanya kwa lengo la kufika mbali na kupeperusha bendera ya Taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...