Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

ALIYEKUWA rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na wenzake wanatarajia kuanza  kujitetea Novemba 20, mwaka huu.

Aveva na wenzake wanakabiliwa na mashitaka ya kughushi na matumizi mabaya ya madaraka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, 

Wakili wa Serikali, Sylvia Mitanto amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa. 

Hakimu Simba amehoji kwanini kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa wakati ilipangwa kwa kusikilizwa? Na Wakili Mitanto amedai katika  shauri lililopita waliitaarifu mahakama kuwa wamekata rufaa kupinga uamuzi wa mahakama hiyo hivyo, wanaomba tarehe nyingine kusubiri uamuzi wa rufaa.

Baada ya kutoa taarifa hiyo, Hakimu Simba amesema watapanga tarehe ya kusikilizwa kwa utetezi na kama kutakuwa na masuala ya rufaa waijulishe mahakama.Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba amehairisha kesi hiyo hadi Novemba 20, mwaka huu kwa utetezi.

Mbali na Aveva washitakiwa wengine ni makamu wa rais, Geofrey Nyange maarufu Kaburu na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hansppope wamekutwa na kesi ya kujibu katika mashitaka saba na kuondolewa mashitaka mawili ya utakatishaji fedha.

Katika mashitaka ya kwanza,  Aveva na Kaburu wanadaiwa kula njama ya kutenda kosa la matumizi mabaya ya madaraka.

Inadaiwa Aveva na Kaburu wanadaiwa kutumia vibaya madaraka yao kwa kuandaa fomu ya kuhamisha fedha Dola za Marekani 300,000 kutoka kwenye akaunti ya Simba iliyoko benki ya CRDB Azikiwe kwenda kwenye akaunti binafsi ya Aveva iliyoko benki ya Barclays.

Pia inadaiwa Aveva na Kaburu  wanadaiwa kwa pamoja kughushi nyaraka iliyokuwa ikionesha Simba inalipa mkopo wa Dola za Marekani 300,000 kwa Aveva kitu ambacho sio kweli.

Aveva anadaiwa katika benki ya CRDB anadaiwa kutoa nyaraka ya uongo ikionesha Simba wanalipa mkopo wa Dola za Marekani 300,000

Aveva anadaiwa kuwa katika Benki ya Barclays Mikocheni alijipatia Dola za Marekani 187,817 wakati akijua zimetokana na kughushi.

Kaburu anadaiwa kumsaidia Aveva kujipatia Dola za Marekani 187,817 kutoka kwenye akaunti ya Simba wakiwa wanajua fedha hizo zimetokana na zao la kughushi. 

Aveva, Kaburu na Hans Poppe  wanadaiwa kughushi hati ya malipo ya kibiashara wakionesha kwamba nyasi bandia zilizonunuliwa na Simba zina thamani ya Dola za Marekani 40,577 huku wakijua kwamba siyo kweli

Katika mashitaka ya nane, Aveva anadaiwa kuwasilisha hati ya malipo ya kibiashara ya uongo  kwa Levison Kasulwa  kwa madhumuni ya kuonesha kwamba Simba wamenunua nyasi bandia zenye thamani ya Dola za Marekani 40,577

Aveva, Kaburu na Hanspope wanadaiwa kuwasilisha nyaraka za uongo kuonesha kuwa Simba imenunua nyasi bandia zenye thamani ya Dola za Marekani 40,577.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...