Na Karama Kenyunko, globu ya Jamii.


ZOEZI la kuomba msamaha na kukiri shtaka dhidi ya kesi ya utakatishaji inzayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi  wa zamani wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathmini wa Takukuru, Kulthum Mansoor limeshindwa kufikia mwisho kufuatia majadiliano kati yake na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), kugonga mwamba baada ya pande hizo kushindwa kufikia muafaka.

Wakili wa utetezi, Elia Mwingira amedai hayo leo Novemba 12,2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Kevin Mhina wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Amedai Oktoba 30, mwaka huu waliieleza mahakama kwamba mteja wake ameandika barua kwa DPP kuomba kuingia makubaliano na kukiri makosa yake na kwamba mazungumzo ya pande zote mbli yalifanyika lakini hayana mwelekeo mzuri hivyo, wanaomba kesi hiyo iendelee kama ilivyokuwa awali.

Kufuatia zoezi hilo kugonga mwamba, wakili Mwingira aliiomba mahakama itoe amri ya kusikiliza kesi hiyo haraka ili mshitakiwa apate haki yake kwa wakati kwani yupo ndani kwa muda mrefu na kesi yake haina dhamana.

Mapema mahakamani hapo, wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upalelezi bado haujakamilika ila wataelekeza wapelelezi kuhakikisha wanakamilisha upelelezi katika maeneo yaliyobakia kwa haraka.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 26, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Katika kesi hiyo, Mansoor anakabiliwa na mashitaka  manane ya kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha Sh bilioni 1.477.

Inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Januari 2013 na Mei 2018, mshitakiwa alighushi barua ya ofa ya  Agosti  13, 2003 kwa madhumuni ya kuonyesha kuwa, barua hiyo imetolewa na Halmashauri ya Wilaya  ya Bagamoyo huku akijua kuwa sieeeo kweli.

 Aidha kati ya Januari 2012 na Mei 2017  huko maeneo ya Upanga ndani ya Wilaya ya Ilala, mshitakiwa kwa kudanganya alijipatia Sh milioni 5.2 kutoka kwa Alex Mavika ambaye ni mfanyakazi wa Takukuru kama malipo ya kiwanja  kilichopo Kijiji cha Ukuni Bagamoyo.

Pia inadaiwa kati ya tarehe hizo,  Mansoor alijipatia Sh milioni tatu kutoka kwa Wakati Katondo kama malipo ya kiwanja kilichopo maeneo ya Kijiji cha Ukuni wilayani Bagamoyo mkoani Pwani. Mshtakiwa pia  alijipatia Sh milioni tano kutoka kwa Ofisa wa Takukuru, Gogo Migutah kama malipo ya kiwanja kilichopo eneo hilo hilo.

Katika mashitaka ya tano, inadaiwa Mansoor alijipatia Sh milioni saba kutoka jwa Ekwabi Majungu  ambaye pia ni ofisa wa Takukuru kama malipo ya kiwanja hicho.

Mansoor anadaiwa kati ya Januari 2012 na Mei 2017, maeneo ya Upanga jijini Dar es Salaam, akiwa Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathminu alijipatia Sh milioni saba kutoka kwa John Sangwa kama malipo ya kiwanja cha eneo hilo.

Indaiwa kuwa mshitakiwa akiwa mwajiriwa wa Takukuru, alijipatia Sh milioni tano kutoka kwa Rose Shingela kwa ajili ya malipo hayo.

Katika mashitaka ya utakatishaji fedha,  inadaiwa kati ya Januari 2013 na Mei 2018 huko maeneo ya Upanga, mshitakiwa  alijipatia Sh1,477,243,000 wakati akijua kuwa  fedha hizo ni haramu na ni zao la kosa tangulizi la kughushi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...