Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeifuta kesi ya Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ya kutaka kusitisha mchakato wa kumuondoa madarakani na kuamriwa walipe garama

Hatua hiyo imekuja leo Januari 13, 2020 baada ya Mwita kupitia wakili wake Hekima Mwasipo kuwasilisha maombi ya kuondoa kesi hiyo mahakamani mbele ya Hakimu Mkazi Janeth Mtega kwa sababu anaona aina tena maana ya kuendelea kuwepokwa sababu maombi yao ya zuio yalishatupiliwa mbali na hajapewa haki ya msingi ya kusikilizwa.

Akiwasilisha maombi hayo, Wakili Mwasipo ameieleza Mahakama miongoni mwa sababu zao ni kwamba anaona kesi hiyo haina maana kuwepo mahakamani kwa sababu hatua za kumng'oa madarakani zilishafanyika na muombaji (Mwita) hakupewa nafasi ya kusikilizwa mahakamani.

Aidha aliomba mahakama kuondoa kesi hiyo bila gharama kwa kuwa haijafika mwisho.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali Rashid Mohammed alidai hawana pingamizi na maombi hayo ila wanaomba suala la gharama liwepo kwa sababu wamepoteza muda, rasilimali na uandaaji wa majibu waliyokuwa wakiyawasilisha mahakamani hapo kuhusu shauri hilo.

Pia Mwasipo alisisitiza kuwa gharama walizotumia upande wa Mashtaka ni kodi za wananchi na Mwita pia ni mwananchi anayelipa Kodi kwa msingi huo aliomba iondolewe pasipo gharama.

Akitoa uamuzi huo Hakimu Mtega amesema "Mahakama imekubali kuliondoa shauli hilo kwa gharama".

Meya Mwita, amefikia uamuzi huo baada ya uamuzi uliotolewa na Mahakama hiyo ya Hakimu Mkazi Kisutu Januari 10,mwaka huu kutupilia mbali ombi la Meya Mwita la kuitaka itoe zuio la muda ili asiondolewe kwenye nafasi yake kwa mpaka pale kesi ya msingi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

Katika uamuzi huo mdogo, Hakimu Mtega alisema haikuona uthibitisho mahakamani hapo juu ya uwepo wa kikao cha kumuondoa madarakani Meya huyo wala hasara atakayoipata endapo ataondolewa.

Kwa upande wa Kesi ya msingi, Mwita anapinga kudaiwa kupendelea madiwani wa chama chake katika uundaji wa kamati mbalimbali bila kumshirikisha Mkurugenzi wa Jiji, kutumia gari la ofisi vibaya na kushindwa kufanya matumizi ya hisa za Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA).


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...