Na Woinde Shizza,  Michuzi TV Arusha
 
Walimu wa shule binafsi nchini wamelalamikia kutokushirikishwa katika usimamizi wa mitihani ya kitaifa pamoja na usahihishaji  licha ya kuwa nguzo muhimu katika maendeleo ya elimu nchini na kuchangia katika kukuza  ubora wa elimu.
Akizungumza katika Mkutano wa Chama cha Walimu wa  Shule binafsi nchini ,Katibu Mkuu wa Chama hicho Julius Mabula mkutano uliofanyika juzi(jana ) katika ukumbi wa golden rose jijini Arusha   ameiomba serikali iwashirikishe katika kusimamia na kusahihisha mitihani ya kitaifa kwani kwa miaka mingi wamekua hawashirikishi licha ya kuwa  na sifa stahiki kama walimu wa shule za serikali
 
“sisi tunasifa kama vile walimu wengine wa shule za serikali wanazo lakini kinachotushangaza atushirikishwi katika swala lolote la usahihishaji mitiani wala usimamizi  wa hii mitiani kwa ufupi naweza sema tumetegwa sisi  walimu wa shule binafsi “Julius Mabula
 
Alisema kuwa watafurahi sana kuona kwamba serikali inatambua uwepo wa kwa kuwashirikisha katika mambo mbalimbali ya uhusuyo elimu  kwani nguzo muhimu katika maendeleo ya ellimu  ni kushirikiana na kuchangia kukuza ubora wa elimu

 Kwa upande wake mgeni rasmi wa mkutano huo Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha  Richard Kwitega alisema kuwa serikali imepokea maombi ya walimu wa shule binafsi katika kusimamia mitihani ya kitaifa na watayafikisha kwenye ngazi husika ili yaweze kufanyiwa kazi

“tumesikia maombi yenu na tumeyapokea na napenda kuwahaidi kuwa tutafikiksha maombi haya katika ngazi husika ili yaweze kufanyiwa kazi hivyo niwaambie usiwe na hofu kwani serikali yenu ni sikivu na itafanyia kazi haya “alibainisha Richard Kwitega

Kwa upande wake Rais wa chama wa walimu wa shule binafsi nchini  Cornel Bukolo hicho pamoja na wadau wa elimu wamesema kuwa walimu wa shule binafsi wanapaswa kushirikishwa katika mipango ya kuboresha elimu na kupatiwa mafunzo ili kukuza kiwango cha elimu na kufikia nchi yenye uchumi wa kati .

  Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha  Richard Kwitega   akiongea katika mkutano huo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...