
Na Amiri kilagalila-Njombe
Askari watatu wa jeshi la polisi mkoani Njombe wamefariki dunia leo baada ya kutokea ajali iliyohusisha basi la kampuni ya Sharoon linalofanya safari zake Njombe -Arusha na kuligonga gari la polisi lililokuwa mbele yake.
Kamishna msaidizi wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema basi hilo lenye namba namba T349 CXD limegonga gari la polisi lililokuwa mbele yake lenye namba PT 3734 toyota land cruser na kusababisha vifo vitatu na majeshuhi tisa.
Kamanda Issa amesema majeruhi wanaendelea na matibabu katika hospitali ya kibena na askari watatu wamefariki wakati wakipelekwa kwenye matibabu.
“Katika ajali hiyo majeruhi ambao walikuwa wamezidiwa zaidi ni watano,mmoja anayetambulika kwa jina la kijeshi namba H 1839 PC Dickson huyu amepata maumivu ya shingo na maumivu mengine mwilini,na amepewa rufaa ya kwenda Muhimbili na hawezi kupanda gari labda usafiri wa ndege hivyo mpaka sasa hivi tunafanya utaratibu askari huyu aweze kusafirishwa kwa matibabu na taratibu zote za kumpeleka zimeshakamilika”alisema Kamanda Issa
kamanda issa amesema askari waliofariki kwenye ajali hiyo kuwa ni namba H 4401 Mariharus Said Hamis mkazi wa lindi, namba H 6802 pc Michael Muhando mkazi wa Geita na H7486 pc Henry Athmani Soka mkazi wa Arusha na Kilimanjaro.
Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya mji wa Njombe dkt Alto Damas Mtega amesema wamepokea majeruhi tisa na miili mitatu ambao wamefikishwa kwaajili ya matibabu majira ya saa kumi na mbili na dakika 10
“Tumepata majeruhi leo ambao wametokana na ajari na wote walikuwa ni askari polisi ilikuwa ni saa kumi na mbili kama dakika kumi ,walikuwa wanatoka kituoni wanaelekea kazini,kwa hiyo tumepata jumla ya majeruhi 7 lakini pia watatu walikuwa wamepoteza maisha,jumla kwenye gari walikuwa watu kumi na mbili na wawili hali zao sio nzuri sana watahitaji kupewa rufaa”alisema Damas Mtega
Majeruhi wa ajali hiyo Mustapha Said amesema namna ilivyotokea hawezikuelezea kutokana na mshtuko uliotokea na kushindwa kuelewa namna ilivyokuwa.
“Tuliona tu gari imepigwa kwa nyuma na watu wote walikuwa wamesharuka kwa hiyo pale hatukuweza kutambua kitu chochote”alisema Mustapha Said
Miili ya marehemu hao inatarajiwa kusafirishwa kesho saa saba mchana kuelekea nyumbani kwa marehemu hao kwaajili ya mazishi.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...