Na Karama Kenyunko, globu ya jamii
MAHAKAMA Ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga Machi 10, mwaka huu kutoa hukumu ya kesi ya uchochezi dhudi ya viongozi nane wa Chadema akiwemo  Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho,Dk.Vicent Mashinji ambaye hivi karibuni  amehamia CCM.
 Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba amesema sheria inaelekeza pande zote kufanya majumuisho ili kuisaidia mahakama kutoa uamuzi kwa kuangalia masuala ya kisheria yaliyoibuliwa wakati wa usikilizaji wa kesi hiyo na wametoa maelekezo kwa pande hizo kuwasilisha hoja zao katika siku tano za kazi baada ya mahakama kukamilisha uchapaji wa nyaraka zilizopo kwenye kesi hiyo na kuwapatia.

Amesema, anatambua kesi hiyo inamvuto kwa jamii, hivyo ni lazima iishe ili kila mmoja aweze kuendelea na shughuli zake na kuongeza  "Majumuisho ya mwisho mnatakiwa muyawasilishe siku tano za kazi," amesema Hakimu Simba. Ameongeza kesi hiyo inakurasa zaidi ya 1,000 ambazo anatakiwa kuzipitia na kutoa hukumu hivyo hukumu ya kesi hiyo itatolewa Machi 10, mwaka huu saa 4:30 asubuhi.
Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Naibu Katibu mkuu wa Chadema upande wa Zanzibar, Salum Mwalimu,  Katibu Mkuu Chadema na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.

Jumla ya mashahidi nane wa upande wa mashtaka walifika mahakamani hapo kutoa ushahidi wao ambapo mahakama iliwaona washitakiwa wote kuwa na kesi ya kujibu na walijitetea kwa kuleta mashahidi kumi na tatu.
Mwaka 2018, viongozi hao walifikishwa mahakamani hapo wakikabiliwa  na mashitaka 13 ikiwemo ya kufanya mkusanyiko usiohalali uliosababisha kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT), Akwilina Akwiline.


Washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka 13 likiwemo la kula njama, ambapo wote wanadaiwa kuwa, Februari Mosi na 16, mwaka jana, Dar es Salaam walikuĺa njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko kutawanyika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...