MKURUGENZI wa Uwezeshaji wa Kampuni ya Yapi Markez inayojenga Reli ya kisasa Standard Gauge, Yetkin Genc Mehmet ((54) akitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu baada ya kuhukumiwa kulipa faini ya dola milioni 100 ama kifungo cha miaka mitatu jela

MKURUGENZI wa Uwezeshaji wa Kampuni ya Yapi Markez inayojenga Reli ya kisasa Standard Gauge, Yetkin Genc Mehmet ((54) raia wa Uturuki amehukumiwa kulipa faini ya USD milioni 100 ama kutumikia kifungo cha miaka mitatu gerezani baada ya kukiri shtaka la kushindwa kutoa tamko la fedha USD 84,850 alizokutwa akizisafirisha.

Aidha mahakama imeamuru kutaifishwa kwa fedha hizo zote kuwa mali ya serikali. 

Mehmet ambaye nchini Tanzania anaishi Ilala jijini Dar es salaam amesomewa hukumu yake na Hakimu Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba baada ya kufikishwa mahakamani leo Februari 27 ma kusomewa shtaka moja la kushindwa kuzitolea taarifa fedha alizokutwa kusafiri nazo.

Mapema akisoma hati ya mashtaka, wakili wa Serikali Mkuu Shadrack Kimaro amedai kuwa Februari 13, mwaka huu huko katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere terminal III jijini Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa anaondoka nchini kwenda Instabul Uturuki alikutwa na USD 84,850 ambazo hakuna amezitolea taarifa kwa Idara ya Forodha. 

Mapema akisoma maelezo ya awali kabla ya kusomewa adhabu wakili Kimaro alidai mshtakiwa Mehmet ni raia wa Uturuki na ameajiliwa na kampuni ya Yapi Merkezi  ambayo inashughulika na ujenzi wa reli ya kisasa Standard Gauge hapa nchini Tanzania.

Imedaiwa siku hiyo alikuwa akisafiri kuelekea Instabul Uturuki kwa kutumia ndege ya Turkish namba TK 0604 huku akiwa amebeba mabegi. Akiwa amefuata taratibu zote za uwanja wa ndege akiwa anaelekea kupanda ndege alikutwa na Ofisa wa usalama akiwa na kiasi hicho cha fedha ambazo hakuna amezitolea taarifa. 

Aidha imedaiwa fedha hizo zimehifadhiwa NMB banki kwenye kitengo cha intelejensia. Mahakama pia imeamuru mshtakiwa kurudishwa pasi yake ya kusafiria na tiketi yake ya ndege.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...