Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake Jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Eyal David ameuomba  uongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kutoa ushirikiano kwa madaktari wa Israel watakaotembelea taasisi hiyo hivi karibuni ili kwa pamoja waweze kuainisha mahitaji yaliyopo katika kuboresha huduma za matibabu ya moyo.

Akizungumza na wajumbe wa menejimenti wa JKCI leo Jijini Dar es Salaam naibu balozi Mhe.  Eyal alisema  ushirikiano ulioanzishwa na nchi hizo mbili tangu mwaka 1998 umekuwa wa mafanikio makubwa katika kuokoa maisha ya watoto wenye magonjwa ya moyo hapa nchini.

“Madaktari kutoka nchini Israel waliopo katika hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) iliyopo jijini Dodoma watatembelea hapa, ninawaomba mtoe ushirikiano kwao na kuwaonesha maeneo mbalimbali ya taasisi ili kwa pamoja muweze kuainisha mahitaji yaliyopo nasi tutayapitia  na kuona namna gani tunaweza kusaidia”, alisema Mhe. Eyal.

Naibu Balozi Eyal aliendelea kusema  Israel imekua ikijivunia kuwekeza katika utoaji wa huduma za matibabu ya magonjwa ya moyo kwa watoto na kuahidi kuendelea kushirikiana na JKCI ili kuokoa maisha ya watoto wengi zaidi  wenye matatizo  ya moyo.

 “Tunajivunia kuwekeza katika utoaji wa huduma za matibabu ya magonjwa ya moyo kwa watoto nchini Tanzania kupitia Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete. NInaaminii ushirikiano huu utaendelea na kuleta mafanikio makubwa zaidi katika utoaji wa matibabu ya magonjwa ya moyo kwa watoto”, alisema Naibu Balozi Eyal.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi alimshukuru Naibu Balozi huyo kwa kuwa sehemu ya kuendeleza ushirikiano na kuomba mafunzo yanayotolewa na Israel kwa wafanyakazi wa Tasisi hiyo yaguse pia na kwa wafanyakazi ambao siyo wa kada ya afya.

“Serikali ya Israel imekuwa ikitoa mafunzo mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa wauguzi na madaktari lakini kwa sasa ninaomba pia mtoe mafunzo kwa wafanyakazi wa kada nyingine zilizopo katika Taasisi yetu”, alilisisitiza Prof. Janabi.
  Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake Jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Eyal David akimjulia hali mtoto Nickson Tarimo aliyefanyiwa upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati alipotembelea Taasisi hiyo leo akiwa njiani kuelekea Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) iliyopo jijini Dodoma.
 Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake Jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Eyal David akimpa pole mtoto Andrew Mwanawima aliyelazwa katika wodi ya watoto ya  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Mhe. Balozi David  alitembelea  Taasisi hiyo leo akiwa njiani kuelekea Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) iliyopo jijini Dodoma.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimwelezea Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Eyal David namna ambavyo Taasisi hiyo inavyoshirikiana na  Israel kupitia taasisi ya Save a Child’s Heart (SACH).
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimwonesha Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake Jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Eyal David picha za wajumbe wa kwanza wa bodi ya wadhamini pamoja na menejimenti ya kwanza ya Taasisi hiyo wakati balozi huyo alipotembelea JKCI leo akiwa njiani kuelekea Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) iliyopo jijini Dodoma.
Picha na: Genofeva Matemu - JKCI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...