Na Mwandishi Wetu,Muchuzi Globu ya jamii

JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia Ofisa Biashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro Daniel Maleki(30) kutokana na kutuhumiwa kuchana na kuchoma moto kitabu cha Juzuu Amma  ambacho ni sehemu ya Quran Tukufu.

 Akizungumza leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro William Mutafungwa amewaaambia waandishi wa habari kuwa mtu huyo amefanya kitendo hicho cha kuchoma Juzuu Amma jana Februari 6 mwaka 2020 katika eneo la Uhindini ,Kata ya Kasiki katika na Wilaya ya Kilosa mkoani hapa na kufafanua mtu huyo ni Ofisa Biashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa na Mkazi wa Mtaa wa Mbumi "B" alionekana akichoma kitabu hicho.

Kamanda amesema kitendo hicho cha kuchoma Juzuu Amma kimeonekana kuwakasirisha waumini wa dini ya Kiislamu na wananchi waliokuwa mahali hapo,hivyo kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi wilayani Kilosa."Jeshi la Polisi kwa kuepuka uvunjifu wa amani ambao ungeweza kutokea waliofika mara moja kwenye eneo la tukio na kufanikiwa kumtia mbaroni mtu huyo na kumfikisha kituo cha Polisi Kilosa pamoja na vielelezo ambavyo ni mabaki ya karatasi za kitabu hicho yaliyochomwa,"amesema.

Amesema ,uchunguzi umefanyika na mtuhumiwa amehojiwa kuhusiana na tukio hilo na leo Februari 7 mwaka 2020 amefikishwa Makamaha ya Wilaya ya Kilosa na kushtakiwa kwa kosa la kufanya kitendo hicho cha kuudhi na kukashifu imani ya dini ya watu wengine .

Hata hivyo kwa mujibu wa Kamanda huyo wa Polisi amesema kutokana na mazingira ya tukio hilo Jeshi la Polisi limeiomba Mahakama chini ya kifungu namba 148(5)(d) cha Sheria ya mwenendo wa makosa ya Jinai ,Jinai mshitakiwa wasipewe dhamana kwa ajili ya usalama wake,Mahakama imeridhia ombi la Polisi na mshitakiwa amewekwa mahabusu hadi Februari 20 mwaka huu ambapo shauri lake litakapotajwa tena.

Hivyo mshitakiwa huyo chini ya ulinzi mkali amepelekwa mahabusu ya gereza  la Kibegere wilayani Kilombero na kwamba ufuatiliaji wa kina kuhusu tukio hilo unaendelea kufanywa na askari wa Idara ya upelelezi.

Kamanda huyo wa Polisi amewaomba wananchi wakiwamo waumini wa dini ya Kiislamu kuwa watulivu kwani tayari wameshachukua hatua dhidi ya mtuhumiwa huku akishauri Watanzania kuendelea kuheshimiana na kuthamini imani ya kila mmoja wao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro William Mutafungwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...