*Yasema wadau wameelewa kazi ya GCLA.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) kanda ya ziwa imesema imeongeza ukaguzi wa maeneo ya wachimbaji wadogo wa Madini  Madini kutoka maeneo 100 hadi kufikia 2013 kwa mwaka 2019.

Uwezo huo umeongezeka katika kipindi cha miaka minne ya Rais Dk.John Magufuli ambapo pia uwezo wa utoaji vibali  vya kemikali  kutoka 1,350  kwa mwaka kufikia vibali 2,246 hali ambayo  inaonyesha Wananchi wanafikiwa na taarifa za Maabara hiyo.

Hayo ameyasema  Meneja wa GCLA kanda ya ziwa Bonaventure Masambu wakati ziara ya waandishi wa Habari na Timu ya Maafisa Habari wa Taasisi 17 zilizo ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto katika Kampeni ya Tumeboresha sekta ya Afya kwa kipindi cha miaka minne ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuonyesha mafanikio yaliyopatikana katika  Taasisi zote zilizo chini ya Wizara hiyo.

Masambu amesema  katika sheria ya usimamizi na udhibiti wa kemikali za viwandani na majumbani  namba 3 ya mwaka 2003  inaitaka GCLA kusimamia kemikali katika hatua ya uzalishaji, usafirishaji mpaka utumiaji wake.

“Madhumuni  ya sheria hii ni kulinda afya  ya watu  na mazingira,tunaposimamia sheria hiyo lazima tufanye ukaguzi  ili tuone kama watu wanakiuka ,pia kusimamia watu wanaotumia kemikali zile kama zinawadhuru  kiafya ili hatua stahahiki kuchukuliwa kwa wahusika  mwisho kuwatambua na kuwasajili wote wanaojihusisha na kemikali “amesema.

Masambu  amesema katika  usajili wa wadau wanaojihusisha na biashara ya kemikali imeongezeka kutoka wadau 73 kwa mwaka kufikia wadau 2013.

“Mafanikio hayo yametoakana  namna sheria  inavyosimamiwa zaidi ukiwa ni pamoja na  kuwafundisha wananchi kuhusiana na  matumizi salama ya kemikali.Masambu amesema kuwa wametoa elimu kwa wadau 520 juu ya matumizi sahihi  na salama ya kemikali na katika maonyesho mbalimbali  watu 3,989  wamepata  elimu juu ya kemikali.

Amesema mafunzo waliyoyatoa  yamesaidia kwa kiwango kikubwa watu kufahamu faida ya kutumia kemikali katika uchenjuaji wa madini badala ya kutumia madini ya mercury katika uchenjuaji.

"Watu baada ya kuelewa faida ya kemikali kumekuwa na ongezeko la watumiaji migodini kutoka 183  kufikia  592 kwahiyo watu wanaachana na mercury katika uchenjuaji sasa wanachangamkia kemikali kutokana na elimu tuliyoitoa"amesema Masambu.

Amesema ongezeko hilo limekuwa na faida kutokana na watanzania  wengi kujiingiza katika biashara ya uuzaji wa kemikali kutoka watu  15 hadi  kufikia wauzaji 92 baada ya kuona fursa ya matumizi ya kemikali  yanekuwa juu.

Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano Serikalini Wizara ya afya Gerard Chami alisema mafanikio hayo ya GCLA ni kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanyika katika sekta ya afya.

Chami amesema kampeni ya tumeboresha sekta ya afya imekuwa na mafanikio makubwa hasa katika kuwaeleza wananchi  yote yaliyofanywa ndani ya awamu ya tano katika kuwaletea wananchi huduma bora.
 Meneja wa Kanda ya Ziwa wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) Bonaventure Masambu  akizungumza na waandishi habari wakati wa ziara ya Waandishi wa Habari na Timu ya Maafisa Habari wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto kuangalia mafanikio ya GCLA Kanda ya Ziwa ikiwa ni Kampeni ya Tumeboresha sekta ya afya.
Meneja wa Kanda ya Ziwa wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) Bonaventure Masambu akionesha kitabu Cha ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) namna GCLA inavyotekelezeka katika utoaji wa huduma kwa Wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...