Meneja Masoko wa Benki ya NBC,
Alina Maria Kimaryo ( wa pili kushoto), akizungumza wakati wa droo ya
mwezi Januari ya kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo ambapo jumla ya
washindi watano walijishindia pikipiki mpya kila mmoja. Wanaoangalia
kutoka kushoto ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Masuli
Masudi, Meneja wa Bidhaa za Kuwekeza, Dorothea Mabonye, Meneja Kampeni
ya Malengo, Mtenya Chewa na mmoja wa washindi wa bodaboda wa droo ya
Disemba, Rosemary Kibodya.

Meneja wa Kampeni ya Malengo wa
Benki ya NBC, Mtenya Cheya ( wa pili kulia), akiziungumza kwa simu na
mmoja wa washindi wa droo ya kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo
aliyejishindia bodaboda. Juma ya washindi watano walishinda zawadi hiyo.
Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Wengine kutoka kushoto
ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Masuli Masudi, Meneja
Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo na Meneja wa Bidhaa za Kuwekeza,
Dorothea Mabonye na mshindi wa bodaboda wa mwezi Disemba,

Meneja Masoko wa Benki ya NBC,
Alina Maria Kimaryo (kulia), akikabidhi zawadi ya bodaboda kwa Bi.
Rosemary Kibodya, mmoja wa washindi wa droo ya mwezi Disemba mwaka jana
wa kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo. Makabidhiano hayo
yalifanyika pamoja na droo ya mwezi Januari ambapo jumla ya washindi
watano waliojishindia bodaboda walipatikana. Wengine kutoka kushoto ni
Meneja Tawi la Corporate, Mariam Kombo na Meneja wa Bidhaa za Kuwekeza,
Dorothea Mabonye.

Meneja wa Tawi la NBC Corporate,
Mariam Kombo akikabidhi kadi ya pikipiki kwa Rosemary Kibodya, mmoja wa
washindi wa droo ya mwezi Disemba mwaka jana wa kampeni ya Ibuka Kidedea
na NBC Malengo. Makabidhiano hayo yalifanyika pamoja na droo ya mwezi
Januari ambapo jumla ya washindi watano waliojishindia bodaboda
walipatikana.
……………………………………………………………………………………………………
BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC),
moja ya benki kongwe nchini imeendelea kuboresha maisha ya wateja wake
kwa kuendelea kutoa zawadi mbalimbali kupitia kampeni yake inayoendelea
ya akaunti ya Malengo iitwayo ‘Ibuka Kidedea na NBC Malengo’.
Akizungumza wakati wa droo ya
Mwezi Januari katika droo za kila mwezi za kampeni ya Ibuka Kidedea
jijni Dar es Salaam leo, Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo
alisema kampeni hiyo imeendelea kufanya vizuri tokea ilipozinduliwa
Oktoba mwaka jana, ikishuhudia wateja wa zamani wakiweka amana katika
akaunti zao za Malengo huku wateja wapya wakijiunga na NBC Malengo ili
kujishindia zawadi na kunufaika na manufaa lukuki yanayopatikana
sambamba na akaunti hiyo.
“Tunaposema ‘Ibuka Kidedea’ ni
kweli tunamaanisha, Kwani mjuavyo hadi sasa jumla ya washindi 10
wamejishindia zawadi za bodaboda huku washindi nane wameshinda safari za
mapumziko kwenda sychelles na Serengeti.
“NBC Ibuka Kidedea imekuja
kusaidia watanzania kutimiza malengo yao. Watanzania wana malengo
mbalimbali kila mmoja ana malengo yake, natoa wito kwa wateja wetu na
wasio wateja kujiunga na NBC Malengo ili kutimiza malengo yenu kwa
urahisi na uhakika”, alisema Bi. Maria.
Bi Maria aliongeza kuwaNBC
inajali maisha ya wateja wake na watanzania kwa ujumla na ndio sababu
kila mara imekuwa ikiingiza bidhaa na huduma zinazoendana na kukidhi
mahitaji halisi ya watanzania.
“NBC ni benki ya kizalendo,
tunajua fika mahitaji halisi ya watanzania, tunajua mahitaji ya wateja
wetu, akaunti ya Malengo ya NBC ni moja ya fursa iliyoletwa na NBC ili
kumuwezesha mteja wetu kujiwekea akiba kidogo kidogo ili kutimiza
malengo yake.
“NBC tunataka wateja wetu na
watanzania wawe na utamaduni wa kujiwekea akiba hata Kama ni kidogo
kidogo kwani mswahili wanasema ‘bandu bandu humaliza gogo”, alisema.
Pamoja na hayo meneja huyo
anasema wale wote wanaojiunga na NBC Malengo sio tu kupata nafasi ya
kuibuka kidedea lakini pia wanashuhudia akaunti zao zikipata faida nono
kila mwezi hivyo kuwasaidia kutimiza malengo yao.
“NBC hatuishii kwenye Malengo
tu, tunaposema ‘NBC Daima Karibu Nawe’ tunamaanisha kuwa NBC ipo karibu
na kila mmoja anayehitaji huduma za kibenki, iwe ni akaunti za vikundi,
wanawake, mikopo ya aina mbalimbali, huduma za kibenki kwa
wajasiriamali, wafanyakazi, katika sekta za kilimo na madini, kila
mahali NBC tupo”, aliongeza Bi Maria.
Katika droo ya leo waahindi
watano waliibuka kidedea na kujishindia pikipiki mpya aina ya Yamaha
kila mmoja huku zawadi kubwa ikipangwa kuwa pikipiki ya miguu mitatu
aina ya Toyo itakayotolewa katika droo kubwa inayotarajiwa kufanyika
mwezi ujao.
Mbali na droo hiyo pia mshindi
wa droo ya mwezi Disemba mwaka jana Bi. Rosemary Kibodya wa Dar es
Salaam alikabidhiwa pikipiki yake katika tukio lililoshuhudiwa pia na
wakaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...