Na Said Mwishehe, Michuzi Globu ya jamii


WAKATI Dunia ikiendelea kupambana na virusi vya Corona( COVID-19) Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Profesa Mohame Janab amewaambia Watanzania kuwa kwasasa kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huo ni muhimu zaidi kuliko kitu kingine kwa kuepuka mikusanyiko, mikutano,send of na harusi huku akifafanua ugonjwa huo ni hatari na hauwezi kulinganishwa na aina nyingine ya mafua  au ugonjwa wowote.

Kupitia taarifa yake ambayo ameitumia kwa njia ya sauti katika mitandao ya kijamii kwa lengo la kuelezea kwa kina ugonjwa huo na madhara yake, Profesa Janab ametumia nafasi yake kufafanua hatua kwa hatua kuhusu ugonjwa huo.

"Nitachangia yale ambayo yatasaidia zaidi kuulewa huu ugonjwa na kujua nini cha kufanya, kama Watanzania tuko wapi na huu ugonjwa, swali kubwa ambalo nikakutana nalo kutoka kwa wagonjwa wanaokwenda kwenye kliniki pale katika Taasisi yetu,  wanauliza kwanini taharuki katika Corona wakati ni sawasawa tu na mafua mengine na pia haupo hata kwenye magonjwa 10 yanayoua watu wengi Duniani kama kifua kikuu na magonjwa na Ini.

"Naomba nianze kwa kusema hivi, tuache kulinganisha ugonjwa huu ugonjwa wa Corona na mafua mengine kwasababu .Kwanza hii COVID-19  maana yake ugonjwa huu ulipatikana Desemba mwaka 2019 na ndio maana ya hiyo 19 na kweli vifo  vyake ni asilimia mbili .

"Kwanini huu ugonjwa tunatakiwa kuuona tofauti kabisa na haya mafua mengine, tafiti zote ambazo zimefanywa na nyingine zitachapishwa kwenye majarida ya sayansi makubwa hivi karibuni zinaonesha huu ugonjwa ni mara 10 ya flue ya kawaida, nini sababu ya kuufanya huu ugonjwa kuwa hatari zaidi.

"Kwanza tangu huu ugonjwa umepatikana na tunaongelea miezi mitatu sasa au mitatu na nusu hauna dawa na wala hauna chanjo ,haya magonjwa mengine ya mafua yanayochanjo, njano ya Corona itapatikana baada ya miezi 18 kuanzia leo Machi 21 mwaka huu wa 2020, kwa maana hiyo tunaongelea mwishoni mwa mwezi mwa mwaka ujao ndio chanjo itakapatikana,"amesema Profesa Janab ambaye ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo.

Hata hivyo amefafanua kuwa sisi binadamu na kama Watanzania miili yetu ina kinga zaidi mbili, moja inaitwa Innet ambayo hiyo ni ya kuzaliwa nayo kupitia kwa mama mjamzito aliyeata chanjo au aliugua ,hivyo mtoto anazaliwa na kinga hiyo na kinga ya pili ni inaitwa aqured ambayo  hata haya mafua mengine Watanzania wamekuwa wakiugua na kupona na mara nyingi huwa yanakuja kwa msimu.

"Wewe Mtanzania nikiwemo mimi tunaugua mafua mara kadhaa kwa mwaka na yanakuja kwa msimu, yanaweza kuanza Desemba yakaenda hadi mwezi wa tatu au wa nne yakapotoea. Miili yetu imejenga kinga ya mafua ya kawaida, lakini huu ugonjwa kama nilivyosema awali ndio kwanza umeanza, hivyo miili yetu imeshutukizwa na huu ugonjwa.

"Na kuna kiitu kinaitwa Democrat ,ukitazama mafua ya kawaida inashambulia watoto na watu wazima lakini vifo tunavyoviona kwa wenzetu inashambulia zaidi watu wenye umri uliosogea mbele mwa kuanzia miaka 70 hadi miaka 80 . Na sababu moja inaweza kuwa kinga ya miili inaweza kuwa ndogo , sababu ya nne ambayo ni hatari zaidi huu ugonjwa wa Corona ukikukuta una magonjwa mengine kama shinikizo la damu,moyo,kisukari na saratani uuaji wake uko kwa asilimia 10 ,na wagonjwa 100 wenye magonjwa mengine wakikutwa na Corona vifo vinakuwa vingi zaidi,"amesema.

Profesa Janab amesema kuwa kama inavyoelezwa asilimia 80 ya watu watapata huo ugonjwa wa Corona na watakuwa na dalili ndogondogo za homa na kila kitu watakaa nyumbani wakijilinda na watapona na asilimia 15 watalazwa hospitali kwasababu watakuwa wameugua sana na watahitaji kulazwa kwa ajili ya kupata tiba ambayo sio ya ugonjwa wenyewe watatibiwa na watapona na asilimia tano watahitaji kulazwa kwenye vyumba vya wagonjwa mahututi(ICU), kwasababu watakuwa watahitaji kuwekea mashine ya kupumulia.

Amefafanua na hapo ndipo changamoto inapoanza na yeye kama daktari hiyo inampa wasiwasi sana kwasababu gani hivyo virusi vya Corona vinatabia yaani kama yeye akiwa navyo mwilini ,akikikohoa anaviacha kwenye hewa lakini vikitua kwa mfano kwenye meza,mlango,vyombo vya plastiki vina uwezo wa kukaa mpaka siku tatu na hivyo mtu akigusa anaambukizwa.

Ameongeza pia kuna kundi ambalo limepata vijidudu vya Corona na halina dalili yoyote wanaweza kuambukiza watu wengine kati ya siku saba hadi 14  na mtu mmoja ambaye ameambukizwa huo ugonjwa na hana dalili yoyote anaweza kuambukiza kati ya watu wanne mpaka tisa.

"Sasa nini kinachotisha zaidi katika ugonjwa huu wa Corona na ndio maana nasema huwezi kulinganisha na mafua mengine ya kawaida, huu ugonjwa unaleta kitu kinaitwa capacity presuard inamaanisha pale mwanzo niliposema asilimia 15 watapelekwa hospitali na asilimia tano watahitaji mashine za kupumulia na hapa tatizo linapoanzia ,ugonjwa wenyewe wahudumu wa afya, wauguzi, madaktari na watu wote wanaotoa huduma aidha watakuwa wameugua na kubaki nyumbani au watakuwa kwenye asilimia 15 ambayo watakuwa wamelazwa.

"Au watakuwa kwenye asilimia tano ya kuwekewa mashine ya kupumulia. Sasa mashine ziko chache na ndicho kilichotokea Italia,mpaka jana madaktari 16 wamefariki, asilimia 8.3 ya wauguzi wa afya aidha mfamasia na watoa dawa za usingizi ambao ukijumlisha ni wafanyakazi 2633 wameathirika na huu ugonjwa , sasa Marekani pamoja na maendeleo yote wana vitanda 34 kwa ajili ya wagonjwa mahututi kwa kila wagonjwa 100,000 na Itali wana vitanda 14 vya wagonjwa mahututi kwa kila wagonjwa 100,000.

"Na ndio maana nchi kama Itali na Iran huduma za afya zilikwama  kwasababu vitanda vilikuwa vichache na wahudumu wameugua  ,ndio maana utaona Itali ugonjwa umeanza wiki tatu zilizopota lakini mpaka jana 3600 wamefariki, na wiki iliyopita ilibidi wachukue maamuzi magumu kwa kuondoa mashine kwa wagonjwa wa zamani na kuwawekea wagonjwa wapya na kwa bahati mbaya wagonjwa wengi ndipo walipopoteza maisha ,tumesikia kwa siku moja walikufa wagonjwa 475," amesema Profesa Janab.

Hivyo amesema hali hiyo huenda ikitokea katika nchi ya Marekani na kwani wameanza kutangaza wagonjwa wa Corona siku 11 au siku 12 nyuma na kwamba kama  hawakuchukua hatua sahihi nako watafika huko."Kwasababu hata ukiitazama Marekani yenyewe pamoja na uwezo wake wote wanatakiwa kupima watu 150,000 kwa siku lakini mpaka jana wameweza kupima watu 20,000 tu kwa siku."


NINI USHAURI WAKE KWA WATANZANIA

Pamoja na hatua mbalimbali ambazo zinaendelea kuchukuliwa  Profesa Janab ameshauri kuwa ; "Sasa nini ambacho tunaweza kufanya Watanzania ni rahisi sana ni kuepuka misongamano isiyokuwa ya lazima,mikutan, send off,harusi ,michezo,misikiti ,makanisani na tayari tumesikia viongozi wetu wa dini wanavyosema.

Pia ameshauri uvaaji wa mask na katika eneo hilo ameeleza anajua nalo limechanganya watu wengi na kwamba mask ambayo inazungumzwa ni mask maalum ambayo inaitwa N - 95 ambayo maana N ni namba na ile 95 ni kwamba inazuia vumbi au vijidudu kwa asilimia 95 na ndio maana  ukiona nchi ambazo zimefanikiwa kwa mfano Singapore na Hong Kong wote walivaa mask na sio kuvaa watu wachache kwani waliokuwa kwenye maambukizi ni rahisi kuambukiza wengine kama alivyosema wadudu wanaweza kukaa mpaka siku tatu .

"Jambo lingine wale wanaojisikia mafua, homa ni vema wakaa nyumbani kwa ajili ya kujilinda binafsi  na kisha kutoa taarifa kwa wahusika kupitia namba zilizotolewa lakini cha msingi zaidi ni kuhakikisha unanawa mikono kwa kusafisha mikono na usiguse mkono wako Kusini,hivyo tune mikono  mara nyingi zaid.

"Kinga ndio kitu pekee kinachoweza kutuokoa kwasababu tukija kupata wagonjwa wengi kwa wakati mmoja itakuwa shida sana kuwapa huduma stahiki na hasa kwa kuzingatia watahitaji mashine za kupumulia  na sisi mashine tunazo zenye ubora lakini idadi ikiwa kubwa itakuwa ngumu. Tusitaharuki Serikali inafanya kila jitihada za kukabiliana na ugonjwa huu na sisi kwenye Taasisi zetu ya Jakaya Kikwete,Muhimbili na Mloganzila tunazo mashine zenye ubora mkubwa lakini kinga ni muhimu zaidi ,kwasasa," amesema Profesa Janab.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...