Na Mwandishi Wetu,Michuzi Blog ya jamii

MKUU wa Mkoa wa Katavi Juma Homera amesema pamoja na kuendelea na shughuli mbalimbali za maendeleo ndani ya Mkoa huo kwa sasa wanaendelea na mkakati wa kujenga Kliniki ya Tiba asili kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa Homela ni kwamba wamefikia hatua hiyo baada ya wannanchi wa Mkoa huo na wadau wa tiba asili kutoa ombi hilo na hiyo ni baada ya kuwepo kwa vitendo vya udanganyifu katika utoaji wa tiba asili.

Amesisitiza kwamba  mkoa unakusudia kujenga jengo ambalo litatmika katika kutoa huduma ya tiba ya asili kwa wadau ambao wamekuwa wanajihusisha nayo na sababu kubwa ni baada ya wadau wenyewe kuomba kuwepo na jengo la tiba asili ambalo huduma zitakuwa zinatolewa kwa uwazi na sio uchochoroni.

"Kutokana na uwepo changamoto kwenye eneo hilo hususani matatibu kuna baadhi ya watoa huduma wamekuwa wakipiga ramli chonganishi vichochoroni, hivyo wadau waliamua kushirikisha kuwa ni vema kukawa na jengo ambalo litatumika kutoa huduma za tiba asili na hivyo tuwaondoa udanganyifu na ramli chonganishi mkoani kwetu,"amesema Homera.

Amesema kuwa katika kufanikisha ujenzi huo wamekubaliana wadau kuchanga Sh.milioni 70 hadi Sh.milioni 100 ambazo zitatumika kwenye ujenzi huo na kuongeza mkoa wametenga eneo kubwa tu kwa ajili ya wa kliniki hiyo na watakaotoa huduma ni wale ambao wanaojuzi na wanatambulika ndani ya Wilaya zao.

"Jambo hili sio geni kwani hata nchi za wenzetu ikiwemo ya China na kungineko wanazo kliniki za tiba asili na kwa hapa kwetu tumeshirikisha watalaamu kutoka wizarani kupitia kwa waganga wakuu wa mkoa na Wilaya ambako huku kote wako waratibu  wa tiba asili "amesema Homera

Akifafanua kuhusu michango amesema ni hayari na wala sio lazima na hiyo ni kwasababu wazo limetoka kwa wadau na hivyo wamekubaliana kuwa kila mtu atatoa kile ambacho anaona anaweza na hatimaye kupata kiasi cha fedha ambacho wamekubaliana.

Ameongeza kutokana uzito wa jambo hilo hata Mwenyekiti wa Shirikisho la waganga wa tiba asili nchini yupo mkoani humo kwa ajili ya kuhamasisha wadau kuweza kuchangia na anaamini kliniki hiyo Itakuwa ya mfano.
MKUU wa Mkoa wa Katavi Juma Homera

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...