Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni George Mkuchika
akiwasilisha mbele ya Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa Taarifa ya
Mapato na Matumizi ya Mafungu ya ofisi yake kwa Mwaka wa Fedha
2020/2021, kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Mary Mwanjelwa.
Kikao hicho cha Kamati kimefanyika katika Ofisi za Bunge, Jijini Dodoma.

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya
Utawala na Serikali za Mitaa wakiwa katika kikao cha Kamati ambapo
wamepokea na kujadili Taarifa ya Mapato na Matumizi ya Mafungu ya Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa
Fedha 2020/2021. Kikao hicho cha Kamati kimefanyika katika Ofisi za
Bunge, Jijini Dodoma.

Katibu wa Kamati ya Bunge ya
Utawala na Serikali za Mitaa, Ndugu Chacha Nyakega akitoa ufafanuzi wa
jambo katika kikao cha kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge,
Jijini Dodoma, kulia ni Mwenyekiti wa Kamati, Mhe. Jason Rweikiza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...