Mkurugenzi wa
Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe
akisisitiza umuhimu wa kutumia Dhana ya Afya moja ambayo hujikita
katika kujumuisha sekta zote za Afya katika kujiandaa, kufuatilia na
kukabili magonjwa yanayomuathiri binadamu wakati wa mafunzo kwa timu za
dharura za kukabili magonjwa ambukizi ya mlipuko leo, Jijini Dodoma,
tarehe 17 Machi, 2020.

Baadhi ya
wataalamu wa sekta za Afya kutoka kwa timu za dharura za kukabili
magonjwa ya mlipuko kutoka ngazi ya mkoa na wilaya zilizo mipakani,
wakifuatilia mafunzo ya kukabili magonjwa ya ambukizi ya mlipuko kwa
kutumia Dhana ya Afya moja, wakati wa mafunzo hayo, leo Jijini Dodoma,
tarehe 17 Machi, 2020.

Mratibu wa Mradi
wa ECTAD Tanzania kutoka FAO, Fasina Folorunso akisisitiza umuhimu wa
kuimarisha Afya ya Binadamu kwa sekta za Afya kutumia Dhana ya Afya
Moja, wakati wa mafunzo kwa timu za dharura za kukabili magonjwa ya
ambukizi ya mlipuko leo, Jijini Dodoma, tarehe 17 Machi, 2020.

Mkuu wa Ndaki ya
Mifugo, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine-SUA, Profesa, Amandus Muhairwa
akisisitiza sekta ya Afya ya mifungo na Afya ya Binadamu,
kushirikiana katika kujiandaa, kufuatilia na kukabili magonjwa
yanayomuathiri binadamu wakati wa mafunzo kwa timu za dharura za
kukabili magonjwa ambukizi ya mlipuko kwa kutumia Dhana ya Afya moja
leo, Jijini Dodoma, tarehe 17 Machi, 2020.

Baadhi ya
Wakufunzi na wataalamu wa sekta za Afya kutoka kwa timu za dharura za
kukabili magonjwa ya mlipuko kutoka ngazi ya mkoa na wilaya zilizo
mipakani, wakifuatilia mafunzo ya kukabili magonjwa ya ambukizi ya
mlipuko kwa kutumia Dhana ya Afya moja, wakati wa mafunzo hayo, leo
Jijini Dodoma, tarehe 17 Machi, 2020.

Mkurugenzi wa
Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe
akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa sekta za Afya kutoka kwa
timu za dharura za kukabili magonjwa ambukizi ya mlipuko kutoka ngazi ya
mkoa na wilaya zilizo mipakani, kwa kutumia Dhana ya Afya moja, wakati
wa mafunzo hayo, leo Jijini Dodoma, tarehe 17 Machi, 2020.
********************************
Dhana ya Afya moja ambayo hujikita
katika kujumuisha sekta zote za Afya katika kujiandaa, kufuatilia na
kukabili magonjwa yanayomuathiri binadamu imeendelea kufundishwa kwa
Wataalamu wa sekta hizo za Afya, ikiwa ni Sekta ya Afya ya Binadamu,
Wanyamapori, Mifugo, Kilimo na Mazingira, ili wataalamu hao watumie
dhana hiyo kuimarisha udhibiti wa magonjwa ambukizi kati ya Binadamu na
wanyama ambayo hutokea mara kwa mara katika maeneo ya mipakani kutokana
na kuwepo kwa muingiliano mkubwa kati ya watu na wanyama katika
mazingira yao.
Katika kuimarisha Afya ya
binadamu, Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO),
pamoja na watalaamu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Chuo Kikuu cha Kilimo
Sokoine wamewapa mafunzo wataalamu wa sekta za Afya wanao toka katika
Halmashauri za Mkoa wa Kagera, Rukwa, Katavi, Rukwa na Songwe zilizo
mipakani juu ya namna ya kujiandaa na kukabili magonjwa ambukizi ya
mlipuko kama vile Ugonjwa wa Corona na Ebola kwa kutumia Dhana ya Afya
moja.
Akiongea wakati wa kufungua
mafunzo hayo leo tarehe 17 Februari, 2020, Jijini Dodoma, Mkurugenzi wa
Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy
Matamwe, amebainisha kuwa ushirikiano wa wataalam na sekta za Afya kwa
kutumia dhana ya Afya Moja hivi sasa ni agenda ya dunia nzima. Aidha,
ameeleza kuwa Dhana hiyo imekusudiwa kutumika maeneo ya mipakani
ambapo mwingiliano huo huchochewa na wasafiri kutoka eneo moja kwenda
jingine, ongezeko la watu duniani, mabadiliko ya tabia nchi, utandawazi,
ongezeko la mahitaji ya maji na chakula.
“Mafunzo haya ni muhimu sana
nchini kwa kujenga uwezo wa nchi katika utayari wa kukabiliana na
magonjwa yanayosambazwa na wanyama na kuathiri wanyama na
binadamu.Tanzania tumeabiwa yupo mgonjwa wa Corona19, ambapo Tumeambiwa
mgonjwa anaendelea vizuri na matibabu, na serikali inaendelea kuchukua
hatua za madhubuti za kuhakikisha ugonjwa huu unadhibitiwa ili usisambae
nchini”.
Awali akiongea katika mafunzo
hayo, Mkuu wa Ndaki ya Mifugo, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine-SUA,
Profesa, Amandus Muhairwa amebainisha kuwa sekta za Afya zikishirikiana
katika Kudhibiti magojwa zitasaidia kuimarisha Afya ya Binadamu kwa
kuwa kila sekta itakuwa inachukuwa tahadhari kwa wakati.
Aidha, Mratibu kutoka FAO wa
Mradi wa ECTAD Tanzania, Fasina Folorunso amabainisha kuwa FAO
inaendelea kushirikiana na serikali mya Tanzania kupitia Dawati la Afya
moja katika kujenga uwezo wa kukabiliana na magonjwa ambukizi ya
mlipuko kwenye ngazi ya mkoa na wilaya hususani maeneo ya mipakani.
Katika kuhakikisha watalaam hao
kutoka sekta za Afya wanaweza kutumia Dhana hiyo katika kudhibiti
magonjwa katika maeneo ya mipakani wameweza kujengewa uwezo wa namna ya
kutoa taarifa za milipuko ya magonjwa ambukizi kama vile ugonjwa wa
Corona 19 na Ebola yanapotokea maeneo ya mipakani, namna ya kuunda
vikosi vya kufuatilia na kukabili Ugonjwa, Mawasiliano wakati wa
kufuatilia na kukabili magonjwa hayo kwa kutumia Dhana ya Afya moja,
pamoja na masuala ya kutumia vifaa Kinga Binafsi vya Kitaalamu.
Tarehe 13 Februari 2018,
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa
alizindua Dawati la Uratibu la Afya moja chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu,
likiwa na lengo la kusimamia na kuratibu shughuli za Afya moja nchini.
Kwa kutambua umuhimu huo Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu,
kupitia Dawati la Uratibu wa Afya moja kwa kushirikiana Shirika la
Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) wakishirikiana na USAID,
OIE, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine – SUA wakishirikiana na Chuo
Kikuu cha Kansas cha nchini Marekani waliandaa na kuratibu mafuzo hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...