Msanii gwiji wa muziki wa Country nchini Marekani Kenny Rogers amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 81.
Mwakilishi wa familia yake amesema kuwa "amekufa kwa amani nyumbani kwa kifo cha kawaida".
Rogers alikua juu katika chati ya wanamuziki wa pop na country katika miaka ya 1970 na 1980 ,na alishinda tuzo tatu za -Grammy.
Akifahamika kwa sauti yake ya kipekee na yenye mvuto hasa katika nyimbo zake -The Gambler, Lucille na Coward Of The County, kazi yake ya muziki ilivuma kwa zaidi ya miongo sita
Wakati mmoja alielezea kwa ufupi umaarufu wake kwa maelezo kwamba anaamini kuwa nyimbo zake " zinasema kitu ambacho kila mwanaume anataka kukisemana kila mwanamke anachotaka kukisikia ".
Baada ya kukulia katika hali ya umaskini mjini Houston, Texas, Rogers alianzia kwa kwa kurekodi msururu wa nyimbo za bendi mkiwemo Kenny Rogers na toleo lake la kwanza kabla ya kuzindua rasmi kazi yake mwaka 1976.
Hakupenda ukosoaji wa muziki, lakini alikua ni mmoja wa watu waliofanikiwa zaidi katika muziki wa country wa muda wote na msanii wa 10 manaume aliyeuza sana albamu za nyimbo zake katika historia ya marekani.
Alishirikiana na wanamuziki wengine magwiji wa muziki wa country wakati wa kazi yake ya muziki, ikiwa ni pamoja na Dolly Parton na Willie Nelson.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...