Na Amiri kilagalila,Njombe
Wajumbe wa jumuiya ya tawala za serikali za mitaa (ALAT) mkoa wa Njombe,wametembelea na kuona maendeleo ya ujenzi wa jengo la ofisi ya uthibiti ubora wa shule wilayani humo ambalo Ujenzi wake umekamilika.
Wakiongozwa na mwenyekiti wa ALAT mkoa wa Njombe Mhe,Hanana Mfikwa,wajumbe hao wamepokea taarifa ya ujenzi wa jengo hilo kutoka kwa mthibiti mkuu ubora wa shule wilaya ya Makete Bw, John Kapinga ambae amesema April 2019 serikali ilitoa fedha za kitanzania kiasi cha Tsh, milioni 152 ili kufanikisha ujenzi wa ofisi hiyo.
“April 2019 tulipokea fedha kiasi cha Tsh,milioni 152 kupitia mfumo wa fosi akaunti ambazo zimefanikisha kukamilisha ujenzi wa jengo hili ambalo tayari limekamilika, pia tumetumia mafundi wa hapa Makete kwa kushirikiana na wataalamu wa halmashauri”Johhn Kapinga.
Vile vile wajumbe wa ALAT mkoa wa Njombe wametembelea shule mpya ya sekondari ILUMAKI iliyopo Kata ya Lupalilo ambayo imejengwa kwa kutumia nguvu za wananchi wa vijiji vitano vya Ilevero, Lupalilo, Ugabwa, Mago na Kisinga Wilayani Makete.
Kaimu mkuu wa shule ya sekondari ILUMAKI Cristoms Mturo amesema ujenzi wa shule hiyo ulianza mwezi Mei 2017 na kukamilika mwezi Novemba 2019 na kisha kupata usajili na kuanza kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwezi Januari 2020, hadi sasa Shule hiyo ina wanafunzi 52 wavulana 26, wasichana 26 na walimu watano.
Hata hivyo amesema hadi sasa ujenzi wa shule hiyo umegharimu Tsh, Milioni 173 laki nne na tatu elfu,kati ya hizo nguvu za wananchi ni Tsh,Milioni 110 laki tisa na elfu tatu na Fedha kutoka Serikalini ni Tsh, Milioni Sitini na mbili na laki tano, Ujenzi bado unaendelea.
Hanana Mfikwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Serikali za mitaa (ALAT) mkoa wa Njombe ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Makete kwa kuendelea kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa wilayani humo huku akitoa wito kwa jamii mkoani hapa kujikinga na homa ya CORONA ambayo ni Janga la Kidunia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...