Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akikata utepe kuashiria kukabidhi Magari 12 kati ya 20 kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji (Rufaa) Semistocles Kaijage (Kushoto) akimkabidhi Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama funguo za gari moja kati ya 12 aliyokabidhi Tume ili alijaribishe kuliendesha. Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dr. Wilson Mahera Charles.
. Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akijaribisha kuliendesha gari moja kati ya 12 aliyokabidhi Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Baadhi ya Wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakishuhudia Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akikabidhi Magari 12 kati ya 20 kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Pili, uwekaji wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
 Magari 12 yaliyokabidhiwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama leo tarehe 04 Aprili, 2020 magari mapya 12 kati ya 20 nje ya Ofisi za Tume zilizopo katika Jengo la Wizara ya Mambo ya Nje Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama ameikabidhi Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo tarehe 04 Aprili, 2020 magari mapya 12 kati ya 20.

Magari hayo 12 yatatumika kwenye Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Pili, uwekaji wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Magari Mengine nane (8) yatakabidhiwa baadaye.

Kulingana na ratiba ya Tume, Uboreshaji Awamu ya Pili utaenda sambamba na Uwekaji Wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura (Display) na utafafanyika kwa ‘ruti‘ mbili kwa siku tatu tu.

Ruti ya kwanza itaanzia tarehe 17 hadi 19 Aprili, 2020 kwa mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Tanga, Mara, Simiyu, Mwanza, Shinyanga, Geita, Kagera, Kigoma, na Tabora.

Ruti ya Pili itaanza tarehe 02 hadi 04 Mei, 2020 kwa Tanzania Zanzibar na Mikoa ya Katavi, Rukwa, Singida, Dodoma, Iringa, Mbeya, Songwe, Njombe, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Morogoro, Pwani na Dar Es Salaam.

Baada ya kukabidhi magari hayo 12, Waziri Mhe. Jenista Mhagama iliipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa Awamu ya kwanza “Ruti” zote 14 kumalizika kwa amani na utulivu mkubwa sana.

Waziri pia aliipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa utendaji kazi wake kwa weredi kwa kutumia mfumo wa Uandikishaji Wapiga Kura kwa kutumia mashine zinazotumia mfumo wa alama za kibaolojia kwa wapiga kura (Biometric Voters Registration) ambao mtu hawezi kujiandikisha zaidi ya mara moja.

Pia aliisifu Tume kwa kuruhusu Vyama vya Siasa kuweka Mawakala kwenye vituo vya Uboreshaji wa Daftari la Kudunu la Wapiga Kura na kwenye vituo vya Kupigia Kura siku ya Uchaguzi na pia kutumia masanduku yay a kuwekea kura ambayo ni ya plastiki ambayo unaweza kuona ndani (Transparency) ili kuweka wazi kwa kila kitu kinachofanywa na Tume.
Waziri Mhagama amesema Tume ipo huru kisheria na kwa mujibu wa Ibara ya 74 (11) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinavyoeleza wazi kuwa katika utendaji wake wa kazi haitaingiliwa na Taasisi yoyote hata Vyama vya Siasa.

Waziri Jenister Mhagama alikazia maneneno ya Rais kuwa mwaka huu kuna Uchaguzi na unatakiwa kuwa huru na Haki na kuitaka Tume itekeleze maagizo hayo kwa sababu ndiyo inashughulika na jambo hilo la Uchaguzi na ipoKikatiba na kisheria na ndiyo maana serikali imeiwezesha kwa vitendea kazi ili isikwame. 

Kabla ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji (Rufaa) Semistocles Kaijage kumkaribisha Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama kukabidhi Magari hayo, aliishukuru Serikari na Ofisi yake kwa ujumla kuandaa bajeti na Bunge kuipitisha kwa ajili ya manunuzi ya Magari hayo 20.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...