Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MTOTO
wa miaka 13 amefariki dunia nchini Uingereza mara baada ya kukutwa na
maambukizi ya virusi vya Corona (Covid-19) hospitali King's College ya
Mjini London na ndugu wa mtoto huyo wamevieleza vyombo vya habari.
Mtoto
huyo raia wa Uingereza alifariki dunia siku ya Jumatatu ameelezwa kuwa
ni muingereza mdogo zaidi kufariki kwa virusi hivyo.
Familia
ya mtoto huyo imevieleza vyombo vya habari kuwa mtoto huyo (Ismail
Mohamed Abdulwahab) alianza kuonesha dalili hasa katika kupata shida ya
upumuaji kabla hajapelekwa hospitali.
"Aliwekwa
katika mashine ya kumsaida kupumua baadaye akawa mahututi na alifariki
siku iliyofuata asubuhi" ameeleza mmoja ya wanafamilia.
Mkufunzi wa chuo cha King's College Nathalie MacDermott amesema kuwa;
"Wakati
tukifahamu ni nadra sana kwa watoto kupatwa na Covid 19 ukilinganisha
na watu wazima, visa hivi vimeonesha umuhimu wa sisi sote kuchukua
tahadhari ili kudhibiti kuenea kwa virusi hivi duniani kote" amesema.
Mapema jumanne kifo cha mtoto wa kike wa miaka 12 kilithibitishwa kuwa ni kifo cha mtu mdogo zaidi kutokea nchini Ubelgiji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...