Na Karama Kenyunko,Michuzi TV

MSHTAKIWA Tito Magoti ambaye ni Ofisa wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), amedai licha ya Serikali kupunguza msongamano wa watu katika maeneo mbalimbali nchini ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona, mahabusu wanaishi kwa hofu kubwa kutokana na mlundikano uliopo huko gerezani.

Magoti anashtakiwa pamoja na Theodory Giyani (36) ambaye ni mtaalamu wa Tehama katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.Wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo shtaka la utakatishaji fedha kiasi cha Sh.milioni 17.

Mapema leo Aprili Mosi, mwaka 2020,Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Janeth Mtega kuwa kesi hiyo leo imekuja kwa ajili ya kutajwa.Upelelezi bado haujakamilika, hivyo aliomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Hata hivyo, mshtakiwa Magito ambaye kesi yao ilikuwa ikiendeshwa kwa video conference kutoka gereza la Segerea wanakoishi kama Mahabusu alinyoosha kidole na alipppatiwa nafasi kuongea alidai, wamejawa na hofu sana kutokana na msongamano wa mahabusu waliopo gereza la segerea.

"Jambo hili linafanya tuishi kwa hofu lakininpia tunajisikia kama tumesahaulika ama kupuuzwa katika jitihada za kujikinga na ugonjwa hatari wa Corona" amedai Magoti na kuongeza kuwa, "Tangu kesi hiyo imeahirishwa siku 14 zilizopita mpaka leo hatujapata nafasi ya kuwasiliana sio tu na mawakili wetu bali hata familia zetu ,kujua mke,watoto na ndugu, hivyo tunahisi kutengwa.

"Tunaiomba Mahakama iangalie swala hili na fursa yoyote ya kisheria ambayo ni convenience ya kutuondolea hofu na kusababisha kusahaulika katika nchi yetu"alimedai.

Akijibu hoja hizo, wakili Wankyo amedai tangu kutangazwa kwa ugonjwa wa corona serikali ilitangaza tahadhari mbalimbali na hakuna mtanzania yoyote aliebaguliwa wala kutengwa,gereza limechukua tahadhari ikiwemo kuzuia kuingia kwa wageni hivyo upo utaratibu waliojiwekea wao wa wageni kuingia gerezani.

Hata hivyo Wakili wa Utetezi Fulgence Masawe alidai magereza wanabebeshwa kosa lisilo lao kutokana na uchekeweshwaji wa upelelezi na ukosaji wa dhamana ndio umesababaisha washtakiwa kuwepo ndani hadi leo.

"Tulitegemea tungeambiwa upelelezi umekamilika na kesi imeanza kusikilizwa ombi letu upande wa mashtaka kuliondoa shauri hili mahakamani ambapo watakuwa na uwezo wa kulirudisha muda wowote"alidai Wakili Massawe

"Sasa ni mwezi wa nne hakuna chochote kinachoendelea tunategemea upande wa mashtaka wanaweza kubadili hati ya mashtaka na kuwaondolea mashtaka yasio na dhamana,baada ya upelelezi kukamilika wanaweza kuyaongeza"

Baada ya maelezo hayo Hakimu Mtega aliwataka washtakiwa hao kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya virusi vya corona kwa kufuata miongozo iliyotolewa na kuutaka upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi, kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 15 mwaka huu itakapotajwa. 

Katika kesi ya msingi inadaiwa washtakiwa hao walikuwa wakimiliki programu ya Kompyuta na kufanya kosa la jinai ambapo waliweza kujipatia kiasi cha Sh.17,354,535
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...