Timu ya wataalamu wakiwa ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Ludewa. Katikati ni Mkuu wa Wilaya hiyo Andrea Tsere akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati. Wa nne kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati Prof. Silvester Mpanduji ambae ni Mkurugenzi Mkuu wa SIDO.
Wajumbe wa Kamati wakinawa Maji na sababu kama sehemu ya kujikinga na COVID-19 kwenye Lango la kuingilia ofisi ya Mkuu wa Wilaya Ludewa. Kutoka Kushoto ni Mkurugenzi anaeshugulikia Uchumi na Miradi, Leo Mavuka kutoka TAMISEMI, Prof. Madundo Mtambo Mkumbukwa kutoka TIRDO, Prof. Silvester Mpanduji Mkurugenzi Mkuu wa SIDO na Afisa Madini Mkoa wa Njombe Wilfred Machumu.
Afisa Madini Mkoa wa Njombe Wilfred Machumu kushoto akiwa na Mzee Kisangani karibu na eneo la Kiwanda chake cha kutengeneza zana zitokananzo na madini ya Chuma wakielekea kuwasalimia wajumbe wa kamati yake.
*************************
Na Issa Mtuwa – Ludewa
Timu ya Wataalamu Tisa kutoka Wizara Nne kwa ajili ya kwenda kumkwamua Mjasiriamali Rueben Mtitu maarufu Mzee Kisangani imewasili mkoani Njombe na kuripoti kwa Katibu Tawala wa Mkoa huo na baadae kuelekea wilayani Ludewa na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya (DC) hiyo Andrea Tsere.

Ujumbe huo uliwasili mkoani Njombe juzi Aprili 03, 2020 wakitokea maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dodoma, Dar es Salaam na Mbeya.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Prof. Silvester Mpanduji ambae ni Mkurugenzi Mkuu wa SIDO alimueleza DC kuwa Kamati yake ikiwa kwenye eneo la Mradi wa Mzee Kisangani itaainisha masuala mbalimbali ya Kiuchumi, Kibiashara, Kimazingira na Kijamii, huku ikibainisha viashiria hatarishi vinavyoweza kutokea kwenye mradi huo na namna ya kutatua.

Aliongeza kuwa wataalamu hao wako katika maeneo ya fani mbalimbali zitakazo kidhi kumkwamua Mzee Kisangani katika mradi wake kama serikali inavyokusudiwa. Kamati hiyo itaainisha masuala mbalimbali yanayohitaji katika kumsaidia Mzee Kisangani katika upanuzi wa mradi wake.

Kila mjumbe anajukumu la kufanya na mara baada ya kazi hiyo ripoti ya kazi hiyo itawasilishwa kwa Waziri wa Madini Doto Biteko kwa hatua zaidi.

Kamati hiyo inatekeleza hadidu za rejea zilizotolewa na kikao cha mawaziri kilichokaliwa Machi 30, 2020 katika utekelezaji wa mpango kazi.

Uthubutu na ubunifu wa Mzee Kisangani umepelekea kumshawishi Waziri wa Madini Doto Biteko kuamsha hari ya kumsaidia Mzee Kisangani kutoka hali aliyonayo kibiashara na kufikia ndoto kubwa ya kuwa mfanyabiashara mkubwa huku akibainisha wizara yake kufanya kila linalowezekana kumwezesha kuwa mfanyabiashara mkubwa kupitia zana zake zinazotengenezwa na Madini ya Chuma.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Andrea Tsere, amemshukuru Waziri wa Madini Doto Biteko, kwa maamuzi ya kuundwa kwa timu hii huku akiwapongeza wataalamu hao kwa kuteuliwa kumsaidia Mzee Kisangani.

Ameongeza kuwa wilaya ya Ludewa ina Raslimali Madini za aina mbalimbali yakiwemo Chuma na Makaa ya Mawe huku kilio chake kikiwa ukosefu wa leseni za wachimbaji wadogo huku maeneo makubwa ya uchimbaji yakiwa yanamilikiwa na Shirika la Maendeo ya Taifa (NDC) huku akiwasilisha kilio hicho kwa mmoja wa Wajumbe kutoka (NDC) Dkt. Yohana Mtoni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...