Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
DEREK
Chauvin ofisa wa polisi nchini Marekani amefahamika zaidi tangu Mei 25
mwaka huu na hiyo ni baada ya kutekeleza mauaji ya mmarekani mweusi
George Floyd hadharani kwa kumkandamiza shingo kwa takribani dakika nane
hadi umauti ulipomkuta.
Derek
Chauvin alizaliwa Machi 19, 1976 huko Fayetteville na alihamia
Minneapolis, Minnesota mwaka 2014 na alianza kufanya kazi akiwa ofisa wa
polisi katika idara ya polisi Minneapolis mwaka 2001.
Kabla
ya kufanya mauaji ya George, Derek amewahi kuwa na malalamiko 18
yaliyokuwa yakimkabili akiwa kazini ambapo baadhi ya malalamiko
yaliondolewa kwa kuonywa kinidhamu na kupewa barua za onyo.
Kati
ya mwaka 2006 na 2011 taarifa za kiofisi zinaonesha kuwa Derek alikuwa
na matukio ya matatu ya matumizi mabaya ya silaha likiwemo la kujeruhi
kwa kisu kilichohusisha polisi 6 na tukio jingine lilisababisha kifo.
Baada
ya Derek kutekeleza tukio hilo mkewe Kelly Chauvin alilaani tukio hilo
mbele ya vyombo vya habari na tayari ameshaanza mchakato wa kubadili
jina la mwisho na kudai talaka kwa ndoa yao iliyofungwa June 12, 2010.
Aidha
kwa mujibu wa aliyekuwa mmliki wa ukumbi wa El Nuevo Rodeo Maya
Santamaria aliieleza CNN kuwa Derek na George walikuwa wakifanya kazi ya
ulinzi katika ukumbi huo ambapo George alifanya kazi ya ulinzi siku ya
Jumanne kama mlinzi wa ziada na Derek alifanya kazi hiyo kwa muda wa
ziada akiwa polisi katika ukumbi huo kwa takribani miaka 17.
Hakuna
ndugu wa Derek anayefahamika isipokuwa mkewe Kellie Chauvin, na
imeelezwa kuwa Derek hapatikani katika mitandao ya kijamii kama
Facebook, Instagram, Twitter na YouTube.
Derek
ameharibu kazi yake kwa dakika nane pekee, ni kazi aliyoitumikia kwa
miaka ipatayo kumi na minane licha ya kuwa barua za maonyo na malalamiko
ya kinidhamu kumi na nane na yaliyokuwa yakimkabili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...