Na Karama Kenyunko, Michuzi TV.

RAIA wa Armenia Vardan Mkhitaryan mkazi wa Mbezi jijini Dar es Salaam na Rosemary Mwamezi mkazi wa Makumbusho, wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi, yenye mashtaka saba yakiwemo ya kufanya udanganyifu kwenye mawasiliano ya simu za kimataifa na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya sh.milioni 44.5.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo leo Juni 8, mwaka 2020 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustina Mbando imedai kati ya Oktoba 1, 2019 na Mei 28, 2020 katika maeneo tofauti ya Jiji la Dar es Salaam washtakiwa wote kwa pamoja walikula njama ya kutenda kosa la kufanya udanganyifu kwenye matumizi ya vifaa vya mawasiliano .

Katika shtaka la pili linalomkabili Mkhitaryan pekee imedaiwa kati ya ya Oktoba 10, 2020 na Mei 28, 2020 maeneo ya Mbezi beach jijini Dar es Salaam washtakiwa wote kwa pamoja wakiwa na nia ya kufanya udanganyifu waliingiza na kumiliki vifaa vya mawasiliano vya kielektroniki bila leseni ya TCRA.

Imeendelea kudaiwa kuwa, siku na mahali hapo, mshtakiwa alisimika vifaa vya mawasiliano vya kielektroniki bila leseni ya kuwa na kibali kutoka TCRA.

Pia mshtakiwa huyo anadaiwa kuendesha vifaa vya mawasiliano ya simu kwa kupokea na kuruhusu mawasiliano ya simu ya Kimataifa bila ya kuwa na kibali huku pia katika shtaka la tano imedaiwa kati ya Oktoba 10,mwaka 2019 na Mei 28, mwaka 2020 katika maeneo ya Mbezi beach jijini Dar es Salaam washtakiwa wote kwa pamoja kwa nia ya kukwepa gharama za viwango vya mawasiliano ya simu za kimataifa walifanya udanganyifu kwa kupokea na kuruhusu mawasiliano hayo.

Pia mshtakiwa huyo anadaiwa kutumia vifaa vya kielektroniki kwa kupokea na kuruhu mawasiliano ya simu za kimataifa bila leseni ya TCRA.

Aidha washtakiwa hao wanadaiwa kati ya Oktoba 10, mwaka 2019 na Mei 28, 2020 katika maeneo ya Mbezi beach jijini Dar es Salaam walitumia vifaa hivyo kufanya mawasiliano ya simu za kimataifa bila leseni ya TCRA na kuisabababishia Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na TCRA hasara ya Sh 44,552,175.

Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo kwa kawaida linasikilizwa Mahakama Kuu.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi hadi Juni 18, 2020, washtakiwa wamerudishwa rumande.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...