Na Woinde Shizza ,Michuzi TV- ARUSHA

MAHAKAMA  ya Mwanzo Maromboso jijini Arusha imemkuta na kesi ya kujibu mtuhumiwa wa kesi ya wizi wa sh.milioni saba inayomkabili kijana wa kazi (House boy) William Mlewa(22) anayetuhumiwa kumwibia Mwajiri wake Anjela Kizigha ambaye ni Mbunge wa zamani wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA).

Hakimu Neema Mchomvu anayesikiliza kesi hiyo alidai kuwa Mahakama imemkuta na kesi ya kujibu na kumtaka mshtakiwa kujipanga kwa ajili ya utetezi wake.

Akisoma mashtaka kwa mshtakwa Hakimu alimsomea vipengele vitatu vya utetezi na kumtaka kuchagua kimoja wapo kati ya kujitetea binafsi,kuwa na mashahidi au kukaa kimya jambo ambalo mtuhumiwa alianza kuangua kilio akiomba ahurumiwe yeye bado ni mdogo na baadaye alichagua kukaa kimya na kuiachia mahakama iendelee.

Hata hivyoHakimu alipodai kuwa hukumu ya kesi hiyo itatolewa Juni 19 mwaka huu na kumtaka mtuhumiwa na Mlalamikaji kufika bila kukosa.

Awali Shahidi wa tano ,katika kesi hiyo iliyounguruma mwishoni mwa wiki iliyopita,James Joseph ambaye ni mtunza mazingira kwa mlalamikaji,alidai alimsikia mtuhumiwa akimwambia mlalamikaji yeye ndiye alikuwa akichukua fedha hizo chumbani kwa bosi wake baada ya kumvizia akiwa jikoni.

Alieleza Mahakama  hiyo kwamba siku ya tukio akiwa nyumbani kwa mlalamikaji alikuja William akitokea nje na kuwauliziamama (Mlalamikaji) alipo na baada ya kumfahamisha kwamba yupo stoo ndipo alipomfuata na kumwambia kwamba amsamehe yeye ndiye ameiba fedha hizo.

Alisema kuwa alimuona mlalamikaji akitokea kwenye chumbani cha stoo akiwa ameongozana na mtuhumiwa huku Mlalamikaji akimtaka Wiliamu kueleza maneno aliyomwambia.

"Ndipo nilipomsikia mtuhumiwa akimwomba msamaha Mlalamikaji akidai kwamba yeye ndiye ameiba fedha hizo na ghafla nilimwona mtuhumiwa akiinama na kutumbukiza kichwa kwenye Sufuria la uji wa Moto na kuunga vibaya,"amedai Shahidi huyo.

Hata hivyo mzee mmoja wa baraza alimuuliza Shahidi iwapo alishuhudia Mtuhumiwa akiiba fedha hizo,jambo ambapo shahidi alishindwa kuthibitisha.

Kea upande wa  shahidi wa sita  Amon Ngairo(32)ambaye ni fundi bomba alieleza kuwa alimsikia Mtuhumiwa akimweleza Mlalamikaji kuwa yeye ndiye amekuwa akiiba fedha hizo kwa kumvizia akiwa ametoka chumbani kwake.

Kesi hiyo imehairishwa hadi Juni 19, mwaka huu siku ambayo mahakama hiyo itatoa hukumu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...