Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald
Kusaya leo (08.06.2020) amefanya ziara ya kushtukiza kwenye eneo la
ujenzi wa vihenge vya kisasa (silos) mjini Shinyanga na kuelezea
kutoridhishwa na kasi ya ujenzi huo .
"
Mkandarasi sijaridhishwa na kazi yako kuwa na kasi ndogo wakati
serikali inahitaji mradi huu wa maghala ukamilike kwa wakati.Nataka
uongeze idadi ya vibarua na mafundi ili spidi ya kazi iongezeke "
alisema Kusaya
Katibu
Mkuu huyo ameelekeza mkandarasi kuwa ataendelea kutembelea ujenzi wa
vihenge hivyo mara kwa mara bila taarifa kukagua kwani Wizara inataka
kuona vihenge na maghala hayo yanakamilika kwa wakati kwa ajili ya
kuhifadhi mazao ya chakula kwa matumizi ya Taifa.
Kusaya
alibainisha kuwa serikali inatekeleza mradi huo mkubwa wa shilingi
Bilioni 15.24 wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi kwa kujenga vihenge (silos)
sita zenye uwezo wa kuhifadhi tani 20,000 na ghala moja kubwa lenye
uwezo wa kuhifadhi tani 10,000 za nafaka katika eneo la Ibadakuli mkoani
Shinyanga.
Katibu Mkuu
Kusaya alikuwa njiani kutoka Mwanza kuelekea Dodoma aliposimama mkoani
Shinyanga kukagua mradi huo wa ujenzi wa vihenge .
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya (aliyevaa
t-shirt mistari nya blu) akikagua eneo la ujenzi wa vihenge vya kisasa
eneo Ibadakuli Shinyanga.Katibu Mkuu huyo ameeleza kutoridhishwa na kasi
ya ujenzi na kutaka mkandarasi aongeze spidi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...