Katika muendelezo wa kutoa  huduma bora za kifedha nchini. Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Halotel kupitia huduma zake za kifedha za HaloPesa, inatarajia kutoa Gawio kwa wateja wake.

Hatua hiyo ikiwa ni hatua ya kwanza kwa HaloPesa kutoa gawio kiasi cha shilingi bilioni moja kwa wateja  wake Zaidi ya Milioni 1.9  ambao ni pamoja na wateja binafsi, mawakala na washirika wake mbalimbali wanatumia huduma za HaloPesa.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar Es Salaam, Mkuu wa kitengo cha biashara cha HaloPesa , Magesa Wandwi alisema “Wateja watapata sehemu ya Gawio hili linalotokana na faida iliyozalishwa kutoka katika akaunti za HalotePesa Trust zilizoko katika mabenki mbalimbali nchini kati ya Oktoba 2016 na Disemba 2018.

Magesa alisema kuwa faida hiyo ni haki ya wateja na hivyo HaloPesa inashauku na furaha kubwa ya kuwalipa wateja wao gawio  hilo kwa mujibu wa sheria ,kanuni  na miongozo mbalimbali kutoka benki kuu ya Tanzania.

"Gawio hili ni la kwanza kwa wateja wetu, na litatolewa ndani ya mwezi mmoja toka sasa, kiasi cha gawio ambacho mteja wa Halopesa atakipata anaweza kutumia atakavyo ikiwa ni pamoja na kutoa au kufanya miamala mbalimbali".alisema Magesa.

"Tunapenda kuwasihi wateja wetu kuwa Halotel tunaendelea na tutaendelea kutoa huduma bora zenye gharama nafuu nchi nzima na waendelee kutumia huduma zetu za HaloPesa",alibanisha Magesa.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara HaloPesa, Magesa Wandwi akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar,akitoa ufafanuzi kuhusu Halopesa Gawio ambapo  Wateja wa HaloPesa watapata sehemu ya Gawio linalotokana na faida iliyozalishwa kutoka katika akaunti za HalotePesa Trust zilizoko katika mabenki mbalimbali nchini kati ya Oktoba 2016 na Disemba 2018.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...