NA MWAMVUA MWINYI
KAMPUNI
ya Mamba Cement chini ya Kampuni Mama ya MM Steel, imetumia kiasi cha
sh.milioni 500 kutengeneza Matenki 2,000 ya kuhifadhia maji ikiwa ni
mkakati wa kupambana na ugonjwa wa Corona.
Matenki
hayo yaliyosambazwa nchi nzima kwa maana ya Tanzania Bara na upande wa
Visiwani, Bara yamepatiwa matenki 1000 katika taasisi za Serikali,
taasisi binafsi 500 wakati Tanzania Visiwani wakinufaika na matenki 500.
Hayo
yalibainishwa na Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Aboubakary Mlawa, akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya
kumkabidhi Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Zainab Kawawa,
matenki 17 kwa ajili ya shule za Sekondari na Vyuo wilayani hapa.
Alisema
,baada ya janga la ugonjwa huo waliwasiliana na Serikali kupitia ofisi
ya Waziri Mkuu, ili Kampuni iweze kuyatengeneza matenki hayo kisha
kusambaza katika maeneo hayo, zikiwemo na ndoo za maji tiririka,
mabeseni pamoja na sabuni.
"Kampuni
yetu imekuwa wadau wakibwa wa Serikali katika kusaidia nyanja
mbalimbali, mara kadhaa tumekuwa mstari wa mbele kusaida katika majanga
na miradi ya kimaendeleo nasi pasipo ajizi tunaungana katika masuala
husika," alisema Mlawa.
Akizungumza
baada kupokea matenki hayo, Kawawa alishukuru Kampuni hiyo kwa
ushirikiano mkubwa wanaoupata kutokea kwenye ofisi hizo, ambapo imekuwa
na msaada mkubwa katika shughuli tofauti za kimaendeleo.
Aliongeza
kwamba baada ya kuwepo kwa ugonjwa huo wa Corona, walimwandikia barua
Mkurugenzi Patel wakimuomba msaada wa matenki hayo yatayosambazwa kwenye
shule na vyuo, malengo makubwa yakiwa kupambana na ugonjwa huo.
Akishukuru
kwa niaba ya walimu wa shule za sekondari kidato cha tano na sita
pamoja na vyuo, Mwalimu Victoria Kesi Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Uktubi na
Uhifadhi wa nyaraka alianza kuishukuru ofisi ya Mkuu wa wilaya kwa
juhudi zake, sanjali na uongozi wa Mamba Cementi kwa msaada huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...