
Mawe makubwa mawili ya
Tanzanite moja lina kilo 9.2 ambalo lina thamani ya shilingi bilioni 4.5
na la pili lina kilo 5.8 lenye thamani shilingi bilioni 3.3.

Afisa Madini akionyesha moja ya jiwe la Tanzanite lilipatikana
Katibu Mkuu Wizara ya Madini Profesa Simon Msanjila amesema kuwa leo Wizara inamtabua Mchimbaji mdogo wa
madini ya Tanzanite Bw. Saninniu Laizer kuwa bilionea baada ya kupata
mawe makubwa mawili yenye thamani ya shilingi bilioni 7.8.
Katibu
Mkuu amesema kuwa mchimbaji huyo amepata mawe hayo mawili ambapo moja
lina kilo 9.2 ambalo lina thamani ya shilingi bilioni 4.5 na la pili
lina kilo 5.8 lenye thamani shilingi bilioni 3.3.

Mchimbaji mdogo wa madini ya Tanzanite Bw. Saniniu Laizer bilionea mpya Tanzania
“Na utofauti wake ni kwamba
mawe ya uzito huo hayajawahi kupatikana kwenye machimbo ya tanzanite
tangu machimbo yaanze na yamepatikana ndani ya ukuta wa Mirereni kwahiyo
hii ni rekodi mpya ya kupata mawe yenye uzito huo” amesema Prof.
Msanjila
Profesa Msanjila amesema kuwa
sekta ya madini inauwezo wa kumfanya mtu kuwa bilionea kwa haraka,
ameongeza kuwa kunahitaji kuwa uwekezaji wa dhati katika sekta hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...