Waziri
wa Madini Doto Biteko akiwa kwenye mgodi wa Irasaniro Buhemba
akizungumza nao kuhusu mambo mbalimbali kuhusu shuguli za uchimbaji na
matukio ya vifo kwenye mgodi.

Mchimbaji mdogo wa Madini Paulo
Ayuke akitoa kero kwa Waziri wa Madini Doto Biteko alipotembelea kwenye
mgodi wa Irasaniro Buhemba.

Waziri wa Madini Doto Biteko na
viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mara wakiongozwa na mkuu wa Mkoa Adam
Malima wakati wakiagana na Waziri wa Madini Doto Biteko.
****************************
Na Issa Mtuwa – Wizara ya Madini,Mara
Vifo vya Wachimbaji wadogo Wawili
wa madini na majeruhi Nane vilivyotokea katika kijiji cha Magunga Wilaya
ya Butiama, vimemfadhahisha Waziri wa Madini Doto Biteko. Waliofariki
ni Kisambi Daudi (30) Mwikizu, mkazi wa Magunga wilaya ya Butiama na
Marwa Mwita Magige (48) Mkurya mkazi wa Nyaburundu wilaya ya Bunda
wamefariki usiku tarehe 11/06/2020 katika mgodi wa Irasaniro Buhemba
mkoani Mara baada ya kufukiwa na kifusi na kuokolewa wakiwa wamefariki
huku waliofariki wamehifadhiwa katika kituo cha Afya Nyamuswa.
Biteko amesema chanzo vya vifo
hivyo ni kutokana na ukaidi wa wachimbaji wadogo kutofuata maelekezo ya
wataalamu wa madini. Amesema eneo lilitokea vifo hivyo lilizuiliwa na
Mkurugenzi wa Migodi nchini Dkt. Abdruhamani Mwanga kutoka Tume ya
Madini alietembelea eneo hilo siku chache zilizopita na kuzuia eneo hilo
lichichimbwe kabla ya vifo hivyo kutoke.
Biteko ameongeza kuwa, pamoja na
katazo hilo wachimbaji hao walikwenda usiku na kuanza kuchimba. Katika
tukio hilo Mkuu wa kituo cha Polisi Buhemba Inspekta Maige alijeruhiwa
kwa kupigwa na jiwe kichwani wakati akiwatawanya wachimbaji waliokuwa
wamekusanyika kwenye eneo hilo kwa ajili ya usalama wao.
Akizungumza kwa ukali na huzuni
akiwa mgodini hapo leo tarehe 12/06/2020 Biteko amesema ukaidi wa
kutofuata sheria na utaratibu unaotolewa na wataalam wa madini ni
ctatizo kwa wachimbaji wa madini. Ameongeza kuwa endapo wachimbaji hao
wasinge kaidi maelekezo ya wataalamu madhara hayo yasingetokea.
“Ndugu zangu mnataka nini kutoka
Serikali hii, maelekezo tuliyopewa na Rais tumetekeleza. Maeneo ya
uchimbaji tumewapa, kodi lukuki tumepunguza, kero tumezitatua, mabobu ya
kukimbizana kati ya Wachimbaji wadogo na wawekezaji katika utawala huu
hakuna, awafanyie nini Rais John Pombe Magufuli…?
Wataalam wa madini walishaweka
tahadhi kuhusu eneo hilo lakini wachimbaji mmekaidi na haya ndio matokeo
yake” alisema Biteko huku akihuzunishwa.
Anasema, kazi yake kubwa ni
kutekeleza anachoagizwa haswa ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali ili
fedha hizo zikatatue changamoto ya wananchi na kuleta maendeleo ya
watanzania wote. Amesema Wizara yake siku zote anaongelea kuhusu Namba
(takwimu) lakini sio Namba za vifo ndo maana anahuzunishwa na vifo
hivyo.
Kufuatia hali hiyo Biteko ametoa
maagizo ni marufuku uchimbaji wa madini wakati wa usiku na kuiagiza
ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Butiama na kamati ya ulinzi na usalama
kuhakikisha uchimbaji wa usiku haufanyiki na atakae kamatwa achukuliwe
hatua ya kisheria.
Eneo la mgodi wa Buhemba kumekuwa
na matukio ya vifo vya wachimbaji wadogo na machimbo hayo yalishawahi
kufungwa kutokana na wachimbaji kufukiwa. Ufunguaji wake uliendana na
utekelezaji wa masheriti waliyopewa ingawaje vifo hivyo vimetokea eneo
jingine lakini hapo hapo Buhemba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...